Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
LIPULI ya Iringa imeweka hai matumaini ya kurejea Ligi Kuu, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Villa Squad jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A, Daraja la Kwanza.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee Lawama Honore Mabena dakika ya 21, kijana mwenye umri wa miaka 19 ‘aliyeichafua’ vizuri ngome ya Villa kabla ya kusukuma mpira nyavuni.
Kwa ushindi huo, Lipuli inatimiza pointi 11 baada ya kucheza mechi sita na kupanda nafasi ya tatu nyuma ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na Majimaji ya Songea, zote pointi 12.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Friends Rangers imeendelea wimbi la ushindi baada ya kuichapa Tesssema mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Iddi Ismail dakika ya 17 na Eliuta Justin dakika ya 44.
Rangers sasa inaendelea kukabana koo kileleni na Majimaji katika viya kuwania Ligi Kuu msimu ujao.

![]() |
Beki wa Lipuli, Hamisi Shaaban Likwena akiupitia mpira miguuni mwa winga wa Villa Squad, Abdul Muharammi wakati wa mchezo baina ya timu hizo jioni ya leo Uwanja wa Karume |
Mchezo mwingine wa ligi hiyo, Friends Rangers imeendelea wimbi la ushindi baada ya kuichapa Tesssema mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Iddi Ismail dakika ya 17 na Eliuta Justin dakika ya 44.
Rangers sasa inaendelea kukabana koo kileleni na Majimaji katika viya kuwania Ligi Kuu msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment