• HABARI MPYA

    Wednesday, November 05, 2014

    MTIRO ALIYEFUKUZWA YANGA KITAMBO AITWA STARS YA NOOIJ, YUMO NA BEKI KINDA WA SIMBA HASSAN ISIHAKA, KIEMBA NA CHANONGO WOTE NDANI

    Mkongwe Abubakar Mtiro
    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MKONGWE aliyewahi kuchezea Yanga SC, Abubakar Twaha Mtiro amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.  
    Mtiro alianza kuchezea Stars mwaka 2000 kama mshambuliaji, baadaye klabu yake ya wakati huo, Yanga SC ikaanza kumtumia kama beki wa kushoto na hakuwahi kuitwa timu ya taifa kwa ajili ya nafasi hiyo- hii ni mara ya kwanza.
    Aliachwa Yanga mwaka 2009 na kuna wakati alipumzika soka kabla ya kurudi uwanjani miaka miwili iliyopita msimu huu, akijiunga na Kagera Sugar ya Bukoba.
    Abubakar Mtiro wa pili kushoto alipumzika soka kwa miaka kadhaa badaa ya kuchwa Yanga SC

    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
    Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
    Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
    Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
    Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIRO ALIYEFUKUZWA YANGA KITAMBO AITWA STARS YA NOOIJ, YUMO NA BEKI KINDA WA SIMBA HASSAN ISIHAKA, KIEMBA NA CHANONGO WOTE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top