• HABARI MPYA

    Friday, November 14, 2014

    SUAREZ AIFUNGIA URUGUAY KATIKA SARE YA 3-3 NA COSTA RICA KABLA YA KUFA KWA PENALTI

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameisaidia Uruguay kupata sare ya 3-3 dhidi ya Costa Rica mjini Montevideo, lakini wenyeji walifungwa kwa penalti 7-6 baada ya Johan Venegas kufunga bao la kusawazisha dakika za mwishoni.
    Nyota huyo wa Barcelona alifunga mapema kipindi cha pili baada ya Alvaro Saborio kuwafungia wageni bao la kuongoza.
    Bryan Ruiz akawafungia Costa Rica bao la pili ndani ya dakika ya moja baada ya Suarez kufunga, lakini mabao mawili ndani ya dakika tatu kutoka kwa Jose Gimenez na Edinson Cavani yaliisogeza Uruguay karibu na ushindi. 
    Luis Suarez scored early in the second half, but Uruguay were denied by a late equaliser from Costa Rica, who won on penalties
    Luis Suarez aliifunga bao la kusawazisha Uruguay ikipata sare na Costa Rica, iliyoshinda kwa penalti
    The £75m Barcelona forward equalised for Uruguay at the beginning of the second half in Montevideo
    Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 75 Barcelona aliisawazishia Uruguay kipindi cha pili Montevideo

    Suarez, ambaye alichaniwa kipande cha jezi, alifunga penalti ya kwanza ya Uruguay, lakini Celso Borges akakosa ya Costa Rica.
    Baada ya kufunga penalti sita mfululizo, Arevalo Rios alipata nafasi ya kuipa ushindi Uruguay, lakini mkwaju wake uliokolewa na kipa wa Real Madrid, Keylor Navas.
    Huku timu hizo zikiwa zimefungana penalti 6-6, Guzman Costa Rica pia ilishinda 3-1 timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Kundi D Kombe la Dunia mjini Fortaleza.

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2834031/Uruguay-3-3-Costa-Rica-Luis-Suarez-leads-second-half-comeback-South-Americans-denied-late-Johan-Venegas-equaliser.html#ixzz3J0QSqH4h 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AIFUNGIA URUGUAY KATIKA SARE YA 3-3 NA COSTA RICA KABLA YA KUFA KWA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top