• HABARI MPYA

    Tuesday, November 11, 2014

    TOTO LA BECKHAM LAMWAGA WINO ARSENAL LICHA YA CHELSEA NA MAN UNITED KUMTAKA PIA

    KINDA Brooklyn Beckham ameripotiwa kusaini Mkataba wa kujiunga na akademi ya Arsenal licha ya Chelsea na klabu ya zamani ya baba yake, David, Manchester United kumtaka pia.
    Mtoto huyo mkubwa wa Nahodha wa zamani wa England alitakiwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England, lakini kinda huyo wa umri wa miaka 15 inafahamika amechagua Arsenal baada ya kuwavutia makocha Kaskazini mwa London.
    Brooklyn amekuwa akifanya mazoezi na The Gunners na kuchezea kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 16, baada ya awali kuchezea Chelsea, United, Queens Park Rangers na Fulham.
    Brooklyn Beckham ameripotiwa kusaini Arsenal licha ya kutakiwa na Manchester United na Chelsea
    Brooklyn is the eldest son of former England captain David Beckham, who played for La Galaxy for five years from 2007
    Brooklyn ni mtoto mkubwa wa Nahodha wa zamani wa England, David Beckham
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOTO LA BECKHAM LAMWAGA WINO ARSENAL LICHA YA CHELSEA NA MAN UNITED KUMTAKA PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top