• HABARI MPYA

    Sunday, April 19, 2015

    ‘CHUI’ WATOZWA USHURU KENYA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    BAO lake Mganda Allan Kateregga liliwafaidi Ushuru FC kuwalaza AFC Leopards maarufu kama Chui 1 – 0 kwenye mchuano wa ligi kuu Kenya, KPL, uliyosakatwa alasiri ya Jumamosi uwanjani Nyayo.
    Mchezaji huyo ambaye alitokea SC Victoria Universityya Uganda na kujiunga na Tusker FC mwaka 2011 kabla ya kwenda zake Nakuru AllStars, St. Joseph FC kisha Bidco United kabla ya kujiunga na Ushuru mapema mwakani alicheka na nyavu dakika ya 57 akimalizia pasi mufti ya Mohammed Hassan ambaye ni mchezaji wa zamani wa Leopards.

    Allan Kategera wa KRA alifunga bao jana

    Hii ilikuwa mechi ya pili Zdravko Logarusic kupoteza katika mechi nane alizoiongoza Chui. Awali walitoka sare tasa na Chemelil Sugar mechi ya ufunguzi, wakapiga droo ya 1 – 1 dhidi ya Thika United na Gor Mahia, kapoteza 0 - 1 baina ya Ulinzi Stars na kuwalabua City Stars 1 – 0 na hatimaye Nakuru AllStars na KCB FC 3 – 1 mtawalia.
    Mabingwa hao mara 13 wa ligi kuu kwa sasa wanashikilia nafasi ya sita kwenye jedwali la timu 16 kwa alama 12 sawia na Ushuru anapochezea Mzalendo David Naftali Tevelu japo wanazidiwa na idadi ya mabao ndiposa watozwa Ushuru hao kushikilia nafasi ya nane.
    Katika mtanange wa awali uwanjani humo, City Stars ilisajili ushindi wa kwanza msimu huu kwa kuwachapa KCB FC 3 – 1 shukrani kwa magoli yake Oscar Mbugua na mawili kutoka kwa chipukizi Ebrima Sanneh huku Raymond Murugi akiipa KCB lake la kuvutia machozi.

    Kwingineko kwenye ligi ya Azam TV na Shirikisho la Soka Kenya, FKF PL, matokeo ya mechi za Jumamosi yalikuwa hivi;
    Kakamega Homeboyz 2 – 1 Ligi Ndogo SC – Bukhungu Stadium
    Modern Coast Rangers 1 – 0 St. Joseph FC – Mombasa Stadium
    FC Talanta 1 – 3 Posta Rangers – MISC Kasarani

    RATIBA YA MECHI ZA JUMAPILI FKF PL
    Bidco United Vs Finlays Horticulture – Thika Stadium – LIVE ON AZAM TV
    Nakumatt FC Vs Zoo Kericho – MISC Kasarani
    Oserian FC Vs Kariobangi Sharks
    Agrochemicals FC Vs West Kenya – Bukhungu Stadium
    Nairobi Stima Vs Shabana FC – Machakos

    RATIBA YA KPL JUMAPILI
    Gor Mahia Vs Sofapaka – City Stadium
    Mathare United Vs SoNy Sugar – Nyayo Stadium
    Chemelil Sugar Vs Thika United – Muhoroni Stadium
    Western Stima Vs Tusker FC – Kisumu
    Nakuru AllStars Vs Ulinzi Stars – Afraha Stadium
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘CHUI’ WATOZWA USHURU KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top