• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2015

    PIGO LINGINE MAN CITY, KOMPANY NDIYO AMEMALIZA LIGI

    TIMU ya Manchester City imepata pigo lingine kuelekea mwishoni mwa msimu baada ya kubainika Nahodha wake, Vincent Kompany anaweza kukosekana kwa sehemu yote iliyobaki kumalizia msimu.
    Beki huyo tegemeo alitilewa katika kipigo cha 4-2 Jumapili kutoka kwa mahasimu, Manchester United - matokeo ambayo yamezima ndoto zao za kutetea ubingwa na sasa wanawania japo kucheza Ligi ya Mabingwa.
    Na kocha aliyekalia kuti kavu, Mchile, akizungumza kuelekea mechi ya kesho dhidi ya West Ham United, amesema Kompany anaweza asionekane tena msimu huu.
    Vincent Kompany is not guaranteed to return this season after injuring himself in the Manchester derby
    Vincent Kompany hana uhakika wa kurejea uwanjani tena msimu huu baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Manchester United

    "Ameumia,' amesema Pellegrini. "NI vigumu sana kwa sasa Ana maumivu ya misuli. Hatujui ni wiki ngapi. Hatujui kama atakuwa fiti kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO LINGINE MAN CITY, KOMPANY NDIYO AMEMALIZA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top