REAL Madrid imeendelea kuifukuzia Barelona katika mbio za La Liga baada ya usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Malaga Uwanja wa Bernabeu.
Kwa ushindi huo, Real inatimiza pointi 76 baada ya kucheza mechi 32, ikiendelea kukaa nafasi ya pili, nyuma ya Barca yenye pointi 78 za mechi 32 pia.
Sergio Ramos alifunga bao la kwanza dakika ya 24, kabla ya Cristiano Ronaldo kugongesha mwamba penalti, ambayo ilisukumwa nyavuni na James Rodriguez dakika ya 69.
Juanmi akaifungia bao la kufutia machozi Malaga dakika ya 71, lakini Mwanasoka Bora wa Dunia, Ronaldo akasahihisha makosa yake kwa kuifungia Real bao la tatu dakika ya 90.
Gareth Bale na Luka Modric wote waliumia kwenye mchezo huo na kutolewa nje.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Pepe, Ramos, Marcelo, Arbeloa/Carvajal dk76, Kroos, Rodriguez, Modric/Illarramendi dk60, Isco, Ronaldo na Bale/Hernandez dk5.
Malaga: Kameni, Angeleri, Roseles, Boka, Sanchez, Amrabat, Garcia, Recio/Damian Tissone dk75, Castillejo/Horta dk81, Darder/Duda dk87 na Juanmi.
Ronaldo alikosa penalti, lakini amefunga bao moja katika ushindi wa it 3-1 dhidi ya Malaga
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3045097/Real-Madrid-3-1-Malaga-Sergio-Ramos-James-Rodriguez-net-Cristiano-Ronaldo-misses-penalty-La-Liga-victory.html#ixzz3XhEdZxfX
0 comments:
Post a Comment