• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    SUAREZ APIGA MBILI BARCA IKIITUNDIKA PSG 3-1 PARIS

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez usiku huu amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 ugenini wa Barcelona Robo Fainali ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Parc Des Princes mjini Paris, Ufaransa.
    Katika mchezo huo mtamu na wa kusisimua, Neymar alikata utepe kwa kuifungia Barcelona dakika ya 18, akimalizia kazi nzuri ya Lionel Messi
    Luis Suarez akafunga bao la pili kwa jitihada za binafsi, akimnyanyasa beki David Luiz kabla ya kuwahadaa mabeki wengine wawili na kutumbukiza mpira nyavuni dakika ya 67. 
    Suarez tena akawainua vitini mashabiki wa Barca baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 79 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Javier Mascherano.
    Gregory van der Wiel akaifungia PSG bao la kufutia machozi dakika ya 82, kuelekea mchezo wa marudiano Aprili 21.  
    Kikosi cha PSG kilikuwa; Sirigu, Van der Wiel, Marquinhos, Silva/Luiz dk21, Maxwell, Rabiot/Lucas dk65, Cabaye, Matuidi, Lavezzi, Cavani na Pastore. 
    Barcelona; Ter Stegen, Montoya, Pique, Mascherano, Alba, Busquets, Rakitic, Iniesta/Xavi dk53, Suarez, Messi na Neymar. 
    Suarez runs away to celebrate his goal as he joined by his ecstatic team-mate Neymar (right)
    Luis Suarez akikimbia kushangilia huku akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Neymar (kulia) usiku huu

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3040576/Paris-Saint-Germain-1-3-Barcelona-Suarez-double-Neymar-target-supreme-Spaniards-ease-victory-Laurent-Blanc-s-given-glimmer-hope-late-goal.html#ixzz3XPkzIap9 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ APIGA MBILI BARCA IKIITUNDIKA PSG 3-1 PARIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top