• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    TOTO AFRICANS YAANZA KUMEGUKA, NAHODHA ERICK NGWENGWE ‘ABWAGA MANYANGA’

    Na Alex Sanga, DAR ES SALAAM
    KIPA namba moja na Nahodha wa Toto African ya Mwanza, Erick Ngwengwe (pichani kulia) ametangaza kuachana na timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
    Kipa huyo anayechukua Shahada ya pili ya elimu kwenye chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, amesema ameamua kuachana na timu hiyo kutokana na mkataba wake uliokuwa ni kuipandisha daraja timu hiyo na baada ya
    kufanya hivyo sasa rasmi ameachana na timu hiyo.
    Ngwengwe amesema kwa sasa amerejea kwenye timu yake ya mtaani, Black Star inayoshiriki Ligi Daraja la Nne na pia amesema kama viongozi wa timu ya Toto watakubali
    matakwa yake, atasaini tena kwenye timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda katikati ya jiji la Mwanza.

    Lakini kuna tetesi zinasema kipa huyo anaelekea Mwadui FC ya Shinyanga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOTO AFRICANS YAANZA KUMEGUKA, NAHODHA ERICK NGWENGWE ‘ABWAGA MANYANGA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top