RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk Patrice Motsepe kwa pamoja na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Burudani ya Saudi Arabia (GEA), wamelitangaza Jiji la Riyadh, Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Super Cup 2024 ya Afrika.
Mechi hiyo ambayo itazikutanisha timu za Misri tupu, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly na mahasimu wao, Zamalek SC na itachezwa Ijumaa Septemba 27, mwaka huu 2024 Jijini Riyadh, Saudi Arabia katika Uwanja ambao utatajwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment