TIMU ya Singida Black Stars imetoa sara ya kufungana bao 1-1 na Stellenbosch ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Stellenbosch ilikuwa ya kupata bao lililofungwa na mshambuliaji mzawa, Langelihle Phili dakika ya 52, kabla ya kiungo wa Kimataifa wa Togo, Marouf Tchakei kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 90’+1.
Kwa matokeo hayo, Stellenbosch wanafikisha pointi nne na kurejea kileleni mwa Kundi C, mbele ya AS Otohô ya Kongo-Brazzaville yenye pointi tatu sawa na CR Belouizdad ya Algeria, wakati Singida Black Stars yenye pointi moja inashika mkia.



.png)
0 comments:
Post a Comment