Barthez |
Na Prince Akbar
KIPA wa Simba, Ally Mustafa ‘Barthez’ ameanza mazaoezi jioni
hii katika klabu yake mpya, Yanga SC kwenye Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam.
Barthez ni miongoni mwa wachezaji 17 ambao hadi sasa tayari wapo
Uwanja Kaunda wakijifua chini ya kocha Freddy Felix Minziro.
Wengine ni Said Bahanuzi na Juma Abdul, wote kutoka Mtibwa Sugar
ya Morogoro na Nizar Khalfan aliyekuwa akichezea Philadelphia Union ya
Marekani- hao ni kwa upande wa wachezaji wapya.
![]() |
Nizar |
Wachezaji wa zamani ambao hadi sasa wamekwishafika Jangwani
ni Juma Seif ‘Kijiko’, ambaye kulikuwa kuna tetesi anakwenda Simba, Hamisi
Kiiza, Kenneth Asamoah, Yaw Berko, Shamte Ally, Jerry Tegete, Stefano Mwasyika,
Godfrey Taita, Athumani Iddi ‘Chuji’, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Idrisa Senga, Omega Seme na Ibrahim Job.
Yanga imeanza mazoezi jana kujiandaa na michuano ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, inayotarajiwa kuanza Julai 14
hadi 29, ikishirikisha na timu nyingine
mbili za Tanzania, Simba SC mabingwa wa Ligi Kuu na Azam FC washindi wa pili.
Yanga ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, baada ya
mwaka jana kuifunga Simba SC kwenye fainali bao 1-0, mfungaji Kenneth Asamoah.
0 comments:
Post a Comment