• HABARI MPYA

    Friday, June 15, 2012

    BREAKING NEWS; DANNY MRWANDA AIGEUKA YANGA, AHAMIA SIMBA, KIGGI MAKASSY AANZA KAZI MSIMBAZI


    Mrwanda
    Na Prince Akbar
    MAKAMU Mwenyekiti wa mabingwa wa Tanzania, Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba wamekamilisha usajili wao kwa kukinasa kifaa kimoja kikali ambacho Yanga walikuwa wanakiwania, ila wakaishia kunawa.
    Ingawa Kaburu hakutaka kutaja jina la mchezaji huyo, lakini uchunguzi wa BIN ZUBEIRY umebaini kwamba, mchezaji mwenyewe ni mshambuliaji wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda ambaye kweli Yanga walikuwa wanamtaka wakashindwana.
    BIN ZUBEIRY inajua Mrwanda aliyewahi kuchezea Simba kabla ya kwenda ughaibuni, atasaini Simba SC wakati wowote kwa sababu mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri.
    Mkataba ambao atasaini Mrwanda ni ambao utamruhusu kuondoka wakati wowote atakapopata timu nje ya Tanzania.
    Pamoja na ishu ya Mrwanda, Kaburu alisema kwamba mchezaji anayefunga usajili wa Simba ni beki wa kati wa kigeni, ambaye bado wanafuatilia uwezo wake ili kujiridhisha.
    Lakini Kaburu amesema mahitaji yote ya Simba yametimia, kwa kusajili winga Kiggi Makassy, washambuliaji Abdallah Juma, Mrwanda, viungo Ibrahim Jeba, Patrick  
    Mbivayanga, Salim Kinje, Mussa Mudde, beki wa kushoto, Paul Ngalema na kupandisha wachezaji watatu wa U-20.
    Aidha, Kaburu alisema ili kuboresha zaidi kikosi, wanafikiria kusajili beki wa kulia kwa sababu Nassor Masoud ‘Chollo’ ni majeruhi wa muda mrefu na kuna uwezekano bahati ikamuangukia beki wa timu hiyo aliyekuwa akicheza kwa mkopo Villa Squad, Haruna Shamte.
    Kaburu
    “Shamte bado kijana mdogo, amecheza msimu mzima Villa Squad na amecheza vizuri, tutamuita mwalimu (Mserbia Milovan Cirkovick) amuone, akiridhika naye, atasajiliwa, Amri Kiemba tumemrudisha tayari, kwa sababu mwalimu alimuona akaridhika naye”alisema Kaburu.   
    Lakini pia Kaburu alisema kwamba wanasaka makipa wawili, kwa sababu kipa wao wa pili Ally Mustafa ‘Barthez’ amesaini Yanga na kipa wa tatu William Mweta ni majeruhi wa muda mrefu pia.
    Wakati huo huo: Kiggi Makassy ameripoti rasmi kazini, kwa mwajiri wake mpya Simba SC na kuanza mazoezi leo asubuhi. “Kiggi ameanza mazoezi rasmi leo,”alisema Kaburu kuhusu kiungo huyo waliyemuiba kwa watani wao wa jadi, Yanga SC. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWS; DANNY MRWANDA AIGEUKA YANGA, AHAMIA SIMBA, KIGGI MAKASSY AANZA KAZI MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top