![]() |
Thadeo, Mkurugenzi wa Michezo |
Na Princess Asia
KONGAMANO linalohusu michezo na amani (National forum on
sport for development and peace) linatarajiwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam,
BIN
ZUBEIRY imeiapta hiyo.
Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi ya Right to Play na British Council
litafanyika kwa siku mbili kesho na keshokutwa, katika hoteli ya Blue Pearl,
Ubungo, Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Idara ya Michezo nchini, Leonard Thadeo
amesema kongamano hilo litawashirika wadau mbalimbali wa michezo kutoka ndani
na nje ya nchi.
Amesema lengo la kongamano hilo ni kutoa fursa kwa wadau
kubadilishana mawazo na kuelezana changamoto zinazoikabili sekta hiyo. Mbali na
kubadilishana mawazo, wadau hao pia wataangalia sera ya michezo nchini na kutoa
ushauri wa nini kifanyike ili kufikia malengo yaliyomo.
0 comments:
Post a Comment