KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kwamba
angepedna kipa David de Gea kuimarika haraka na kumudu kuendana na aina ya mchezo
wa Ligi Kuu ya England.
De Gea amekuwa akipambana ili kumudu kucheza kwa kutumia nguvu
kama inavyotakuwa katika soka ya English gtangu atue klabu hiyo kwa dau la
pauni Milioni 18 msimu huu, akitokea Atletico Madrid ya Hispania.
Pia Sir Alex, anaamini kipa huyo mwenye umri wa miaka 21 ana
dalili zote za kipaji cha kipa mzuri katika vidole vyake na anaweza kuwa
maarufu baadaye Old Trafford.
"Kijana amejaaliwa kipaji. Yuko vizuri, lakini amekuwa
na wakati mgumu wa kumudu kuendana na mchezo wa hapa," alisema Mscotland
huyo.
"Ni suala la kujiendeleza. Anafanya kazi kubwa gym. "Ikiwa
ataimarika kama jiwe, bila kupoteza wepswi wake na kasi, itakuwa babu kubwa
kwake."
De Gea, ambaye mwanzoni alikuwa maarufu kwa kuvurunda,
ameanza kuimarika siku za klaribuni baada ya kusota benchi kwa siku kadhaa.
0 comments:
Post a Comment