BEKI ngongoti Mkenya, aliyewahi kucheza Yanga, Joseph
Shikokoti anatarajiwa kurejea kwao kesho baada ya kufeli majaribio katika klabu
ya Gandzasar FC ya Armenia.
bongostaz imepata habari za ndani kwamba Nahodha huyo wa
Tusker ya Kenya, alishindwa kumvutia kocha wa Gandzasar FC katika mchezo wa
kirafiki aliopewa kama majaribio.
"Shikokoti ni mchezaji mzuri, lakini anafanya makosa
mengina haendani na mfumo wetu wa uchezaji", alisema Mr. Khashmanyan,
kocha wa Gandzasar.
"Tulimpa Shikokoti nafasi ya ajabu, lakini kwa bahati
mbaya, mambo hayakwenda vizuri. Ilikuwa ni uzofu mzuri kwake na tunamtakia kila
la heri katika maisha yake ya soka", alisema Ken Joseph Msemaji wa ETSM,
wakala wa michezo anayesihi London ambaye alimfanyia mpango huo mchezaji huyo.
Shikokoti amekuwa Armenia kwa mwezi na atajiunga tena na Tusker
atakaporejea.
0 comments:
Post a Comment