SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) kupitia bodi yake ya
sheria, (IFAB), Jumamosi itaamua kama timu zitakuwa zikiruhusiwa kufanya
mabadilikio ya wachezaji wanne katika muda wa nyongeza sambamba na mustakabali
wa mstari unaogawa goli na Waislamu kucheza wamefunika vichwa.
Mkutano wa 126 wa IFAB mjini Bagshot, Kusini Magharibi mwa
London, pia utazungumzia adhabu kali zaidi, iliyopewa jina "triple
punishment" ambayo itamhusu mchezaji ambaye atazuia kwa makusudi mpira
unaoelekea kutinga nyavuni, kwamba pamoja na adhabu ya penalti na kadi nyekundu,
pia afungiwe.
IFAB itasikiliza pendekezo la kuongeza idadi ya wachezaji wa
kutokea benchi kutoka watatu hadi wanne mchezo unapofika kwenye dakika 120 kwamba
itaswaidia kuongeza ladha ya mchezo na kupunguza majeruhi.
Bodi hiyo pia itapitia wazo la kutumia teknolojia golini, jambo
ambalo limekuwa mjadala mkubwa kwa kafribu muongo wote huu.
FIFA imesema kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu kutumia teknolonjia
golini utachukuliwa katika mkutano mwingine wa IFAB, unaotarajiwa kufanyika Julai 2, siku
moja baada ya fainali ya michuano ya Euro 2012, mjini Kiev.
IFAB pia itatafakari wazo la kutumia marefa watano, kwa
kuongeza refa mmoja nyuma ya goli kuwasaidia marefa watatu wanaotumika kwa sasa.
Naye Prince Ali wa Jordan, Mjumbe mdogo zaidi kwa umri wa katika
Kamati ya Utendaji ya FIFA, atawasilisha ombi la kutaka wacghezaji wa kike wa
kiislamu waruhusiwe kuvaa hijab, ikiwa ni miakia mitano baada ya vazi hilo
kupigwa marufuku kwenye soka kwa sababu za kiusalama.
0 comments:
Post a Comment