KLABU ya Barcelona itawakosa beki Eric Abidal na kiungo Thiago Alcantara katika mechi ya Ligi Kuu ya Hispania, dhidi ya Sporting Gijon kesho.
Abidal amerejea kutoka kwenye mechi ya kirafiki katikati ya wiki timu yake ya taifa, Ufaransa akiwa majeruhi baada ya kuumia nyonga na kwa hilo Barcelona imesema atakuwa nje ya kikosi kwa siku 10, wakati Thiago atakuwa nje kwa muda usiojulikana baada ya kuumia mguu wake wa kulia akiichezea Hispania.
Ikumbukwe pia Barcelona itamkosa mfungaji wake bora Lionel Messi katika mchezo wa Jumamosi kwa sababu anatumikia adhabu ya tano za njano.
Wapinzani wa Barcelona, Real Madrid wanaongoza La Liga kwa pointi 10 zaidi.
0 comments:
Post a Comment