KLABU ya Schalke imempa ofa Nahodha wa zamani wa Real
Madrid, Raul Gonzalez kuongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Bundesliga.
Meneja Mkuu wa Schalke, Horst Heldt alisema jana kwamba
wamempa Raul ofa ya kuongeza mkataba, ambao unamalizika mwisoni mwa msimu, taarifa
ambayo ametumiwa mwakilishi wake nchini Hispania, Gines Carvajal.
Mkongwe huyo mwenyr umri wa miaka 34, Raul amefunga mabao 25
katika mechi 56 za ligi akiwa na jezi ya Schalke tangu ajiunge nayo mwaka 2010 akitokea
Real Madrid. Amefunga mabao 33 katika michuano yote akiwa na klabu hiyo na Ujerumani,
yakiwemo 14 msimu huu.
Nahodha huyo wa zamani wan Hispania, aliiwezesha klabu hiyo
kutwaa Kombe la Ligi Ujerumani katika msimu wake wa kwanza Schalke, mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment