• HABARI MPYA

    Friday, March 02, 2012

    MAN CITY YASEA TEVEZ BADO MNYELA, APEWA MUDA ZAIDI KUJIWEKA FITI

    KLABU ya Manchester City imempa muda zaidi Carlos Tevez kabla ya kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, kwanza afanye programu maalum ya kujieka fiti, baada ya Muargentina huyo kushindwa kufanya vizuri alipopewa dakika 45 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa milango imefungwa.
    Mshambuliaji huyo ambaye, ambaye hajachezea vinara hao wa Ligi Kuu tangu agome kupasha misuli moto aingie kuichezea City ikiwa nyuma 2-0 mbele ya Bayern Munich Septemba, mwaka jana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, alionekana mchovu aklicheza dakika 45 za kwanza mbele ya Ofisa Utawala wa soka, Brian Marwood na Mkurugenzi wa Maendeleo, Patrick Vieira katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Preston.
    Akiwa nje ya klabu kwa miezi kadhaa, amepumzika nyumbani kwao Argentina, bongostaz inatambua kwamba Tevez anatakiwa kupewa muda zaidi ili kujiweka fiti kwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Bolton katika michuano ya Manchester Senior Cup Jumanne.
    City awali ilitumai kumjumuisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 katika kikosi kitakachocheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Swansea, Machi 11, lakini kutokana na mshambuliaji huyo kucheza ovyo, klabu hiyo sasa imemsogezea mbele muda wa kurejea uwanjani hadi kwenye mechi dhidi ya Chelsea, Machi 19.
    Tevez alisema atahitaji wiki mbili tu za kujifua kabla ya kuanz akazi rasmi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YASEA TEVEZ BADO MNYELA, APEWA MUDA ZAIDI KUJIWEKA FITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top