![]() |
John Bocco 'Adenayor', kinara wa mabao wa Azam |
WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, Azam FC watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu
kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara
ya kwanza mwaka 1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na
timu tatu, nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa
wa Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah
Malabeja amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo, yanaendelea
vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na watatangazwa katika Mkutano
maalum hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment