Boban akisaidiwa na Rage |
MSIBA
wa aliyekuwa mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi Simba Patric Mutesa Mafisango
umewagusa mamia ya watu hapa nchini na hasa wapenzi wa soka na wachezaji kwa
ujumla huku ukimgusa zaidi mchezaji mwenzake Haruna Moshi ‘Boban’ na kupelekea leo mchana kutinga Sigara ambapo mwili wa marehemu ulikuwa ukiagwa bila ya kuwa na
kiatu mguuni.
Mara
baada ya wachezaji wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambao wako kambini katika
hotel ya Tansoma kwa ajili ya kujiwinda
na mechi ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 kwa
kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast kufika katika viwanja hivyo wakiwa
wanashuka katika basi ndipo Boban alishikwa na butwaa mara baada ya kujina yuko
peku.
Aidha
Boban licha ya kuwa peku alijikuta amepanda katika basi hilo huku akiwa
hajapiga mswaki wala kunawa uso ambapo ilipelekea mmoja wa viongozi wa Stars
kutoka uwanjani hapo na kwenda kumnunulia ndala na mswaki.
Boban
alipoulizwa na mmoja wa viongozi kulikoni hata hajavaa viatu wala kunawa uso
alibaki akimtazama huku akijiangalia bila ya kuamini kama ni kweli ameweza
kufika katika eneo hilo bila ya kuwa na kiatu mguuni.
Kiongozi
mwingine wa Stars alifanya jitihada za kuwa nae karibu nyota huyo mpaka
kiongozi mwenzake alipoleta Mswaki na kandambili za bluu ambazo Baban alizivaa
mpaka mwisho wa shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa rafiki yake wa karibu na
mcheziji mwezake katika timu.
Aidha
Boban kutokana na machungu ambayo alikuwa nayo alishindwa kuvumilia kukaa
katika eneo ambalo timu ya Stars ilikuwa imepangiwa kukaa na kunyanyuka na
kwenda kukaa chini karibu na jeneza la aliyekuwa rafiki yake marehemu Mafisango
na kuwafanya watu mbalimbali waliofika katika eneo hilo kuangua vilio.
Mara
baada ya Boban kutinga uwanjani hapo bila ya kiatu mguuni mwandishi wa habari
hizi alimfuata mmoja wa viongozi wa Stars ambaye alisema kuwa licha ya kufika
hapo bila ya viatu ilikuwa wamuache kambini kwa kuwa mara baada ya kupanda
kwenye gari walishangaa hawamuoni na kurudi vyumbani na kumkuta amelala
usingizi kutokana na uchovu mara baada ya juzi kushinda msibani.
Kifo
cha Mafisango kimepelekea Stars Kushindwa kufanya mazoezi siku ya jana asubuhi
na kupelekea kufanya mazoezi jioni kwa kuwa wachezaji wote walitinga Sigara kwa
ajili ya kutoa heshima za mwisho.
0 comments:
Post a Comment