• HABARI MPYA

    Friday, May 18, 2012

    KIKWETE AMLILIA MAFISANGO

    Rais Kikwete
    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage kufuatia kifo cha kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda mwenye silia ya DRC, Patrick Mutesa Mafisango usiku wa kuamkia jana.
    Rais Kikwete amesikitishwa na kifo cha Mafisango katika umri mdogo na amewapa pole wana Simba wote.
    Amesema katika kipindi kifupi cha Mafisango kucheza Tanzania amechangia mafanikio ya soka ya Tanzania kupitia klabu yake, Simba. Mwili wa Mafisango umeagwa leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe na kwenda kuhifadhiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, tayari kusafirishwa kesho kwenda Kinshasa, DRC kwa mazishi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKWETE AMLILIA MAFISANGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top