BAADA
ya kucheza soka kwa miaka 22 mlinda mlango wa zamani wa Arsenal David Seaman
aliamua kustaafu akiwa na umri wa miaka 40 na kuamua kutumia muda wake kwa
ajili ya kufanya shughuli za uvuvi.
Lakini
mwaka 2009, mke wake, Seaman, Debbie, alitangaza kuwa mumu wake huyo ambaye
sasa wameachana alikuwa akimuaga kuwa anakwenda kuvua na kuwinda usiku, lakini
alijiingiza katika kufanya mapenzi kisisiri.
Seaman
mwenye umri wa miaka 45, aliachana na mke wake aliyezaa naye watoto wawili Februari
mwaka 2009, kutokana na tabia mbaya ya mlinda mlango huyo kuwa na mahusiano ya
kimapenzi nje ya ndoa.
Debbie
Seaman mwenye umri wa miaka 47, kwa mara ya kwanza aligundua kama mumewe
‘anacheza mechi za ugenini’ baada ya kukuta picha ya mwanamke kwenye simu Seaman
iliyotumwa kwa njia ya ujumbe.
Mke
huyo alimuuliza mumewe na huyo ambaye walidumu kwa miaka 10 kwenye ndoa yao na
kumjibu kuwa ilikuwa picha ya mwanamke mmoja wa anayeishi Mjini Birmingham na
wala haina maana yoyote akimtaka apuuzie.
Mwanamke
huyo hakutaka kuvunja ndoa yake na kuamua kuendelea kukaa na mumewe ingawa
alipofuatilia juu ya simu hiyo aligundua kuwa Seaman alianza kuwasiliana na
mwanamke huyo tangua mwaka 2005 wakati huo wao walioana mwaka 1998.
Pamoja
na mwanamke huyo ambaye Debbie aligundua kuwa alikuwa ameshafanya mapenzi na
mumewe mara nyingi, pia mumewe huyo alikuwa na mawasiliano kwa njia ya ujumbe
na mwanamke mwingine kwa muda wa miezi mitatu.
Lakini
mlinda mlango huyo aliendelea kumsisitizia mke wake kuwa hakuna jambo lolote
linaloendelea yeye na wanawake hao na mda si mrefu ataacha kuwasiliana nao, ila
mkewe hakuwa akimwamini tena kutokana kuwa na mahusiano na wanawake wawili nje
ya ndoa yake hiyo.
Fabruari
mwaka 2009, Seaman aliondoka nyumbani kwake Hertfordshire muda wa jioni bila
kuacha taarifa yoyote, alipopigiwa simu hakupokea hadi saa 11 alfajiri na
kusema kuwa alikuwa hataki kuoana na mkewe huyo kwa hiyo hana mpango wa kurejea
nyumbani kwake tena.
Baadaye
alirejea nyumbani akiwa na mwanake mwingine aitwaye Frankie Poultney dansa wa
kwenye barafu mwenye umri wa miaka 35 na mkewe alisikia taarifa hiyo kupitia
vyombo vya habari kwamba mumewe ana mpenzi mwingine.
Seaman
na Debbie walianza mahusiano baada ya mlinda mlango huyo kuachana na mke wake
wa kwanza aliyeishi naye kwa miaka 10 pia aliyekuwa akiitwa Sandra.
Nyota
huyo aliyekuwa amepanga kujihusisha kwenye uvuvi na kucheza gofu baada ya
kuacha soka mwaka 2004, mwaka 2006 alionekana kwenye kipindi kimoja cha
Televisheni ya ITV akiwa kwenye kipindi cha ‘live’ cha kudansi kwenye barafu
akiwa na mshirikia wake kwenye mchezo huo Pam O’Connor.
Mpenzi
wake mpya Poultney na yeye alionekana kwenye kipindi hicho kwa mara ya kwanza
mwaka uliyofuata akicheza na mchezaji wa zamani wa Manchester United Lee
Sharpe.
David
Andrew Seaman, alizaliwa Septemba 19 mwaka 1963, Rotherham, Kusini mwa Mji wa Yorkshire
nchini England, amecheza klabu mbalimbali lakini muda mwingi ameutumia akiwa Arsenal
kabla ya kustaafu Januari 13 mwaka 2004, kutoka na maumivu ya bega yasiyopona,
Wakati
akiwa Arsenal alifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali, mataji mataji matatu ya
Ligi Kuu ya England 1991, 1998, 2002, Kombe la FA mara nne mwaka 1993, 1998,
2002, 2003), Kombe la Ligi mwaka 1993 na Kombe la Washindi la barani Ulaya
mwaka 1994.
Kwa
kipidni chake cha soka alicheza kwenye timu ya Taifa kwenye fainali ya Kombe la
Dunia mwaka 1998 na 2002, Mataifa ya Ulaya mwaka 96 na Euro 2000, alicheza
jumla ya mechi 75, akiwa ni mlinda mlango wapili wa England kucheza mechi nyingi
baada ya Peter Shilton.
Seaman
alionyesha kiwango kizuri kwenye timu ya Taifa ya England wakati wa michuano ya
Mataifa ya Ulaya mwaka 1996 na kwa upande wa Arsenal kipindi chake kizuri
kilikuwa ni mwaka ni wakati wa Kombe la UEFA na Ligi Kuu ya England katika
msimu wa mwaka 2002–03.
Na
vipindi vibaya kwa mlinda mlango huyo ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa Kombe la UEFA
kwa klabu yake ya Arsenal alipofungwa bao la mbali kwenye fainali na Nayim na
fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 Ronaldinho alimtungua kwa mpira wa mbali
wa adhabu kwenye hatua ya robo fainali dhidi ya Brazil.
Seaman
alikulia Mjini Rotherham na kusoma shule ya Kimberworth Comprehensive na kuanza
kucheza soka lake kwenye klabu ya Leeds United, lakini klabu yake ilimuunga
mkopno kocha Eddie Gray, ambaye alikuwa hamtaki Seaman, ingawa mlinda mlango
huyo alikuwa akimpenda Gray tangu akiwa mchezaji.
Seaman
aliuzwa kwenye timu ya Daraja la Nne iitwayo Peterborough United Agosti mwaka
1982 kwa ada ya pauni 4,000 na kuanza kujitengenezea jina na baada ya miaka
miwili Oktoba mwaka 1984, alijiunga na timu ya Daraja la Pili ya Birmingham
City kwa pauni 100,000.
Klabu
hiyo ilipanda Ligi Daraja la Kwanza lakini mwaka uliyofuata ikashuka tena na
Agosti
mwaka 1986, Queens Park Rangers walilipa pauni 225,000 kwa ajili ya huduama ya
Seaman na kucheza klabu hiyo iliyokuwa uwanja wenye nyasi za plastiki.
Mwaka
1990, kabla ya mfumo wa sasa wa usajili England kulikuwa na nafasi ya kusajili
wiki chache kabla ya kumalizika kwa msimu, hivyo Arsenal ambao walikuwa ni
mabingwa wa Ligi hiyo mwaka 1989, walitaka kumsajili Seaman.
Mpango
huo ulitaka kumuhusisha mlinda mlango wa Arsenal John Lukic, ambaye alitakiwa
kwenda QPR kwa mkopo ili kubadilishana na Seaman ila Lukic alikataa na dili
likavunjika bila usajili huo kufanikiwa.
Msimu
uliyofuata kocha wa Arsenal wakati huo George Graham, alirejea kwenye klabu
hiyo ya QPR na pauni milioni 1.3 na kumsajili Seaman aliyeweka rekoodi ya
mlinda mlango aliyesajiliwa kwa bei kubwa na kumuacha mlinda mlango wa Arsenal
Lukic aliyekuwa na mashabiki wengi Gunners kujiunga Leeds.
Akiwa
Arsenal Seaman alipata mafanikio makubwa na kutwa mataji mengi, ikiwa ni pamoja
na kucheza msimu wa mwaka 1990–91 na kuruhusu mabao 18 tu katika mechi 38
alizocheza na kutetea taji lao na baada ya Terry Venables kupewa kibarua cha
kuinoa England alimuona Seaman kama chaguo lake la kwanza na mlinda mlango
alibakia kwenye kikosi hicho hadi mwaka 2002.
Mwaka
1995, George Graham alifukuzwa na Arsenal walikaribia kutetea Kombe lao la
UEFA, huku Seaman akionekana kama mchawi wa kudaka mikwaju ya penalti baada ya
kunasa penalti ya Attilio Lombardo wakati wa hatua ya nusu fainali na Gunners
kuwatoa Sampdoria.
Lakini
walifungwa kwenye mchezo wa fainali katika muda wa nyongeza baada ya mchezaji
wa Real Zaragoza Nayim, kufunga bao la umbali wa yadi 45 wakati Seaman akiwa
ametoka kidogo kwenye mstari wa lango lae.
Hata
alipotua Arsene Wenger Agosti mwaka 1996 kuinoa Arsenal, Seaman aliendelea
kupewa nafasi na msimu wa mwaka 1998–99, alicheza mechi zote 38 na kuruhusu
mabao 17 na kwenye nusu fainali ya Kombe la FA, Arsenal walitolewa nje na Manchester United, huku wakifungwa penalti
kwenye fainali ya Kombe la UEFA dhidi ya Galatasaray mwaka 2000 baada ya kutoka
sare ya 0-0.
Seaman
alishinda mataji mawili kwa mwaka 2002, Kombe la FA na lile la Ligi Kuu ya
England, pamoja kumaliza vibaya soka lake kwa upande wa timu ya Taifa kutoka na
umri kuwa mkubwa, aliokoa shambulizi la kukumbukwa msimu wa mwaka 2002–03 katika
mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Sheffield United.
Mchezaji
wa Sheffield Paul Peschisolido alipiga kichwa akiwa ndani ya kiboksi kidogo,
huku Seaman akiwa ametoka langoni kwenda kuokoa mpira wa kona lakini aliruka na
kuugusa mpira huo ambao ulidondoka eneo na hatari na mchezaji mwingine wa
Sheffield akapiga shuti lililokwenda juu, huku zikiwa zimesalia dakika chache
kabla mpira haujaisha na Arsenal kushinda bao 1-0.
Wakati
wa mechi hiyo ya nusu fainali mlinda mlango wa Manchester United wakati huo Peter
Schmeichel, ndiye alikuwa mchambuzi wa mechi hiyo kwenye kituo cha Televisheni
cha BBC na kusifu akisema: “Seaman amefanya kazi ambayo sijawahi kuona mlinda
mlango yoyote akifanya.”
Seaman
amekaa langoni mwa Arsenal kwa muda mrefu zaidi na kuwa mchezaji wa pili
kucheza mechi nyingi baada ya Ray Parlour, mlinda mlango huyo amecheza mechi 325
na Juni mwaka 2008 alitajwa kama mchezaji namba saba kati ya wachezaji 50 wa Gunners.
Alichwa
kwenye klabu hiyo ya Arsenal mwaka 2003 na kujiunga Manchester City chini ya
kocha Kevin Keegan, lakini hakuweza kucheza kwa muda mrefu kwenye klabu hiyo
baada ya kusumbuliwa na majeruhi yasiyopona na Januari mwaka 2004 akiwa na umri
wa miaka 40 alitangaza kuacha soka.
Seaman
alianza kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa mwaka 1988,
baada ya kuitwa na kocha Bobby Robson na Novemba mwaka huo alicheza mechi yake
ya kwanza dhidi ya Saudi Arabia ikiwa ni mchezo wa kirafiki.
Alikuw
amechaguliwa kama mlinda mlango namba tatu akiwa na akina Peter Shilton na Chris
Woods wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990.
WASIFU
WAKE
JINA:
David Andrew Seaman
KUZALIWA:
Septemba 19 mwaka 1963 (48)
ALIPOZALIWA:
Rotherham, England
UREFU:
Futi 6 inchi 3
TIMU
ALIZOCHEZEA:
1981–1982
Leeds United (Academy)
1982–1984
Peterborough United (mechi 91)
1984–1986
Birmingham City (mechi 75)
1986–1990
Queens Park Rangers (mechi 141)
1990–2003
Arsenal (mechi 405)
2003–2004
Manchester City (mechi 19)
JUMLA:
Mechi 731
(Tangu 1988
hadi 2002 aliichezea England mechi 75)



.png)
0 comments:
Post a Comment