Aadhibiwa katika mashindano ya Uhispania
DEREVA wa timu ya McLaren, Lewis Hamilton,
sasa amewekwa kando na hataweza kuwa miongoni mwa madereva ambao wataweza
kupata pointi katika mashindano ya Jumapili ya mashindano ya langalanga ya
Formula One nchini Uhispania, baada ya kuliacha gari lake hatua chache kabla
kituo cha mwisho alipomaliza mashindano.
Hamilton alifuzu kuwa wa kwanza kuanza
mashindano Jumapili, lakini sasa amepangwa katika nafasi ya mwisho.
Aliarifiwa asimame, kwani gari lake
lilikuwa halina mafuta ya kutosha alipokaribia kituo cha mwisho, kwani
kulingana na sheria za mashindano hayo, ni lazima uwe na angalau lita moja ya
mafuta, ili yaweze kukaguliwa.
Maafisa wa mashindano hayo walikataa hatua
ya McLaren ya kujitetea, kwamba ukosefu wa mafuta ni hali ambayo ilimsaidia
Hamilton kujiweka katika nafasi bora zaidi ya mashindano hayo.
Kulingana na kifungo cha sheria kuhusiana
na mafuta, kipengele 6.6.2 juu ya kanuni za kiufundi, kinaeleza kwamba
"washindani wote lazima kuhakikisha kwamba angalau wana kiasi cha lita
moja ya mafuta, ambayo yanaweza kutolewa wakati wowote wakati wa mashindano ili
kufanyiwa ukaguzi".
Sheria hizo pia zinaeleza kwamba
"ikiwa kipimo hicho cha mafuta kitahitajika baada ya kipindi cha
mashindano ya mazoezi, gari linalohusika lazima kuendeshwa kwa nguvu zake
zenyewe hadi kituo", yaani pasipo kusukumwa au kuvutwa.
Sheria za Formula One zinasisitiza kwamba
gari lazima kurudi katika kituo likiwa na angalau lita moja ya mafuta, kwani
kuwa na chini ya kipimo hicho humnufaisha dereva na kujiweka katika hali bora
zaidi ya ushindani akijilinganisha na madereva wenzake.
Ingawa hali hiyo haikumsaidia Hamilton
katika kuongoza katika mashindano ya mazoezi alipomtangulia Pastor Maldonaldo
wa timu ya Williams kwa muda wa sekunde 0.578, wasimamizi wa mashindano
walihisi hawanabudi kuiadhibu timu ya McLaren.
Taarifa ya maafisa hao ilieleza: "Kuna
mtu katika timu aliyeweka mafuta yasiyotosha katika gari, na ikabidi hatua ya
kulisimamisha gari hilo kabla ya kufikia kituo ili kupata kipimo fulani cha
mafuta kwa madhumuni ya kuyakagua".
Kwa upande wake, taarifa ya McLaren
ilielezea: "Tunakiri maafisa wa mashindano hawakukubaliana nasi jinsi
tulivyojitetea kwamba kuhusiana na hali hii, haikutoa nafasi dereva kuweza
kujinyakulia pointi zaidi".
Martin Whitmarsh, mkuu wa timu ya McLaren,
alikuwa amejitetea kwa kuelezea kwamba kutokana na tofauti kubwa ya muda kati
ya Hamilton na dereva Maldonado kutoka Venezuela, Hamilton ilifaa aachiwe
kuanza katika nafasi ya kwanza Jumapili.
"Kulikuwa na tofauti kubwa, na
kulingana na hali ilivyo hivi sasa katika Formula One, hamna shaka
angeliruhusiwa kuwa mwanzo", alilalamika Whitmarsh.
Lakini hayo yalikataliwa, na Maldonado, kwa
mara ya kwanza katika maisha yake, ataanza wa kwanza katika mashindano
Jumapili, na Fernando Alonzo naye wa timu ya Ferrari akisogezwa mbele hadi
nafasi ya pili.
Bila shaka Hamilton atajiuliza ni kwa nini
anakabiliana na tatizo hilo kwa mara ya pili.
Kanuni kuhusiana na mafuta zilibadilishwa
na bodi ya dunia ya mchezo wa mashindano haya, FIA, wakati tatizo kama hilo
lilipompata Hamilton mwaka 2010 katika mashindano ya Canada ya Grand Prix.
0 comments:
Post a Comment