![]() |
Dina Ismail , Mratibu |
WAREMBO watakaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012, kesho wataanza kujinoa kwenye hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika maandalizi ya shindano lao litakalofanyika baadaye mwezi ujao.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ameiambia BIN ZUBEIRY mchana wa leo kwamba warembo hao watatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, pamoja na Ustawi wa Jamii.
“Kesho tutaanza mazoezi yetu pale Lamada ambapo warembo kutoka vyuo vinne wataanza kujinoa…wiki ijayo huenda tukaongeza washiriki wengine ambao watatoa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambao wanafanya shindano lao mwishoni mwa wiki hii,”alisema.
Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya ukufunzi wa mrembo aliyepata kushiriki shindano hilo, Rose John, huku kwa upande wa shoo watanolewa na Bob Rich.
Dina aliwataja wadhamini waliojitokeza mpaka sasa ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, na Dodoma Wine, huku akiomba makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo litakalofanyika mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment