TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars inatarajia kuondoka
nchini Mei 24 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Addis Ababa kwa ajili ya
mechi ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
dhidi ya Ethiopia .
Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.
Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.
Msafara wa Twiga Stars utakuwa na watu 25 wakiwemo
wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
wa Wanawake Tanzania (TWFA)
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Lina Kessy ndiye atakayeongoza msafara huo.
Twiga Stars itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu kusubiri
mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam . Mshindi
ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazochezwa
Novemba mwaka huu nchini Equatorial
Guinea .
Wakati huo huo: mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Twiga Stars na Afrika
Kusini (Banyana Banyana) iliyofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza
sh. 8,012,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 6,418 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo
kwa viingilio vya sh. 1,000, sh. 5,000 na sh. 1,000. Washabiki 6,057 walikata
tiketi z ash. 1,000.
Asilimia 18 ya mapato ambayo ni sh. 1,222,169 ilikwenda
kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa
tiketi (sh. 1,560,000), waamuzi (sh. 650,000), usafi na ulinzi (sh. 1,000,000),
maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing
Construction (sh. 500,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh.
475,966, asilimia 10 ya uwanja sh. 237,983, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) sh. 118,992 na asilimia 65 ya TFF (sh. 1,546,890).
0 comments:
Post a Comment