Friday's gossip column
PSG WAVAMIA MCHEZAJI WA MANCHESTER CITY...
WAMWAGA fedha katika usajili, Paris St-Germain ya Ufaransa wanamfuatilia mshambuliaji mwenye umri wa miaka 27 wa Napoli, Muargentina, Ezequiel Lavezzi, ambaye pia inafikiriwa anatakiwa klabu ya Manchester City, ambayo nayo haina mzaha katika kumwaga noti.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Luis Suarez amesema kwamba atakaribisha nafasi ya kucheza Hispania.
MWANASOKA bora chipukizi wa mwaka Ufaransa, kinda wa miaka 22 kutoka Morocco, Younes Belhanda, amesema kwamba anataka kubaki Montpellier kwa msimu mwingine, licha ya kuhusishwa na mpango wa kutakiwa na Manchester City na Arsenal
MSHAMBULIAJI wa Wolves, Steven Fletcher anatarajiwa kuipiga chini ofa ya kuhamia Sunderland.
WAKATI HUO HUO: Kipa wa Sunderland, Craig Gordon amesema atabakia katika klabu hiyo, licha ya kwamba mkataba wake umeisha mwishoni mwa msimu.
KINDA wa miaka 21 wa klabu ya Bologna, kikungo wa kimataifa wa Uruguay, Gaston Ramirez, ambaye inaaminika anatakiwa na klabu kadhaa England, ikiwemo Liverpool, anaweza kuichezea timu hiyo ya Italia mechi ya mwisho msimu huu, wakala wake amesema.
MAN UNITED HASARA MBAYA
UKAGUZI wa mahesabu wa klabu ya Manchester United wa sasa unaonyesha klabu hiyo imeingia hasara ya pauni Milioni 71 katika fedha zilizowekezwa na mmiliki wa klabu hiyo, Glazers katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.
KAKA wa Theo Walcott, amesema yeye na baba yao hawatakwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 kumuona kipenzi chao, winga wa England akifanya vitu vyake kwa sababu ya kuhofia usalama wao dhidi ya mashambulizi ya kibaguzi.
0 comments:
Post a Comment