Roberto Mancini
Adel Tarabti
KOCHA wa Manchester city Roberto Mancini
anasema ana imani na wachezaji wake kutimiza jukumu lao na kuvishwa kilemba cha
Mabingwa wa msimu huu.
Hata ikiwa watashindwa,Mancini amesisitiza
kua vijana wake wamecheza soka safi msimu huu wa Ligi kuu.
Roberto Mancini amesema: Nawaamini kwa
asili mia 100. Wanafahamu vyema kua ushindi wa Ligi na kuin'goa United kutoka
kilele cha soka ilichoshikilia kwa mda mrefu ni jukumu lao.
Aliongezea kusema kua' wamejitahidi na
kupambana kila wanapoingia uwanjani katika Ligi ambayo ni mojapo ya Ligi kali
duniani.
Mancini amemalizia kwa kusema ninavyohisi
ni kwamba mwishoni ni mshindi ni yule anayestahili ushindi''
Klabu ya City iliongoza ligi kwa pointi 8
na kujikuta nyuma ya mahasimu wao Manchester united kwa pointi 8 baada ya
kufungwa kwenye uwanja wa Arsenal tareh 8 mwezi Aprili.
Manchester City inapambana na QPR kwenye
uwanja wa Etihad huku United ikielekea uwanja wa Brittania kuchuana na
Sunderland.
Mancini anasema kua "nadhani kwa
wakati huu ilikua bora kwentu kupoteza mechi dhidi ya Arsenal, kwa sababu hilo
lilitupunguzia shinikizo''
Daima tumeamini, na kuendelea kucheza soka
safi licha ya kua na matatizo kipindi cha mwezi mmoja tu.
"tulipocheza dhidi ya Manchester
United na Newcastle tulicheza vizuri sana, dhidi ya Timu ambazo ni kubwa na
zinazocheza mchezo wa kiwango cha juu, nadhani hali itakua hio hio dhidi ya
QPR.
Ferguson na Meneja wa QPR Mark Hughes
wamezielezea mbinu za Mancini kama za kuzuia, ambapo Ferguson anadai kua
walipocheza dhidi ya City ilitumia wacheza kiungo watano.
0 comments:
Post a Comment