Irene kushoto akiwa na mumewe, Ndikumana kulia na mtoto wao enzi za mapenzi motomoto. |
MUME wa mwigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya, ambaye ni
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi Stars, Hamadi Ndikumana ‘Katauti’
amerejeshwa kwenye timu ya taifa ya nchi yake.
Beki huyo ambaye amekuwa akifungiwa vioo kwenye timu hiyo
kwa muda mrefu, ameitwa tena kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 32 cha kocha
Milutin Sredojovic ‘Micho’ kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania tiketi
ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2014 nchini Brazil na
Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini.
Ndikumana, mwenye umri wa miaka 33, ambaye amesaini tena Rayon
Sports ya Rwanda iliyomuinua kisoka, baada ya kutemwa na APOP Kinyras Peyias ya
Cyprus mapema mwaka huu, alikuwa miongoni mwa wachezaji maarufu waliounda Amavubi
iliyocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2004 nchini Tunisia.
Akiwa ameichezea mechi 51 Rwanda, beki huyo mzoefu ndiye
mchezaji aliyeichezea mechi nyingi zaidi Amavubi na sasa ana nafasi ya
kujiongezea idadi ya mechi chini ya Sredojovic, kocha wa zamani wa Yanga.
Mara ya mwisho aliichezea Amavubi mwaka 2009 na tangu wakati
huo amekuwa akidharauliwa na makocha mbalimbali kutokana na utovu wa nidhamu, ambao
ulimfanya atofautiane na uongozi wa zamani wa Shirikisho la Soka Rwanda (Ferwafa)
chini ya Brigedia Generali Jean Bosco Kazura.
Sura nyingine mpya kwenye kikosi hicho ni Hamdan Bariyanga wa
Etincelles, Olivier Kwizera wa Isonga na François Hakizimana wa Isonga pia.
Wachezaji hao pamoja na kucheza mechi za kuwania tiketi ya
Brazil 2014 na fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, pia watacheza Kombe la
CECAFA Challenge, ambalo fainali zake za mwisho zilifanyika Dar es Salaam mwaka
jana.
Ndikumana amepitia
misukosuko mikubwa mwaka jana, iliyochangia kuathiri kipaji chake hadi akatemwa
Ulaya- kubwa ni kutofautiana na mkewe, Irene ambaye hivi sasa inaelezwa
wameachana, licha ya kuwa tayari wana motto mmoja.
0 comments:
Post a Comment