TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini, Banyana
Banyana, jioni hii imeitandiika Tanzania, Twiga Stars mabao 5-2 kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa Twiga Stars
inayonolewa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya wanaume, Taifa Stars,
Charles Boniface Mkwasa, baada ya wiki iliyopita kufungwa 4-1 na Zimbabwe
kwenye Uwanja huo huo katika mchezo wa kirafriki pia.
Aidha, haya ni matunda ya programu mbovu ya maandalizi ya
timu hiyo hivi sasa, ambayo mara kwa mara imekuwa ikicheza mechi za kirafiki na
timu ya waigizaji, badala ya kuwekeza kwenye maandalizi thabiti ya kuijenga
timu.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Banyana yalitupiwa nyavuni na
Portia Modise dakika ya 23 na 46, Sanah Mollo dakika ya 73 na 79 na Jamine van Wyk
dakika ya 86, wakati ya Twiga yalifungwa na Fatuma Bashir dakika ya 67 na Asha Rashid
‘Mwalala’ dakika ya 77.
0 comments:
Post a Comment