Warembo mazoezini |
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
“Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
DIWANI wa Kata ya Kigamboni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dotto Msawa, atakuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu ' Redd's Miss Kigamboni 2012' ambalo litafanyika kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanamshukuru diwani huyo pamoja na diwani wa Vijibweni (CCM), Suleiman Mathew, kusaidia maandalizi ya shindano hilo.
Alisema kuwa warembo 12 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanatarajia kuchuana kuwania taji hilo na anaamini kwamba kitongoji hicho kimepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
Aliwaomba mashabiki na wadau wa sanaa ya urembo kujitokeza kushuhudia malkia wa Kigamboni anavyopatikana ikiwa ni shindano pekee lililoko ufukweni wa bahari.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Domotila Shayo.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment