Uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho
alivyotolewa kipa wao namba moja, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao mawili wakati
klabu hiyo ikichapwa 2-0 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodcom Tanzania Bara juzi. Pichani ni Ofisa Habari wa Simba,
Ezekiel Kamwaga akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Mtaa
wa Msimbazi, kulaani vurugu hizo na amesema wanafikiria kuwachukulia hatua kali
watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo. Taarifa zaidi kuhusu mustakabali wa
Simba hivi sasa inakuja. |