• HABARI MPYA

    Wednesday, January 09, 2013

    MIEMBENI KUING'OA TUSKER MAPINDUZI LEO?

    Miembeni itaing'oa Tusker leo?

    Na Mahmoud Zubeiry
    TUSKER FC inashuka dimbani leo usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kumenyana na Miembeni katika Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi.
    Mchezo huo, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, kwani kwa sasa Miembeni ndiyo timu inayoiwakilisha vema Zanzibar katika mashindano haya na inaungwa mkono na Wazanzibari wengi.
    Kocha wa Miembeni Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na leo atawaonyesha kwamba mpira ni zaidi ya nguvu. 
    Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi.
    Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.
    “Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
    Nusu Fainali ya pili itachezwa kesho kati ya Simba SC na Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MIEMBENI KUING'OA TUSKER MAPINDUZI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top