• HABARI MPYA

    Sunday, February 10, 2013

    MALI YAIFUNGA TENA GHANA NA KUTWAA NAFASI YA TATU AFCON


    Malian players celebrate
    TIMU ya taifa ya Mali jana imeifunga mabao Ghana 3-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, wakiipiku Black Stars kwa mwaka wa pili mfululizo kwenye mashindano haya. 
    Mshambuliaji Mahamadou Samassa alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 21, Nahodha Seydou Keita akafunga la pili dakika ya 48 na Sigamary Diarra akahitimisha karamu hiyo ya mabao. 
    Kwadwo Asamoah aliifungia Ghana bao la kufutia machozi dakika ya 82. Mshambuliaji wa Ghana, Wakaso Mubarak alikosa penalti mapema kipindi cha pili. 
    Flying start: Mahamadou Samassa scored the first goal for Mali in Port Elizabeth
    Mahamadou Samassa alifunga bao la kwanza kwenye Uwanja wa Port Elizabeth

    TAKWIMU ZA MECHI

    Kikosi cha Mali: Soumaila Diakite, Diawara, Salif Coulibaly, Adama Coulibaly, Tamboura, Ousmane Coulibaly, Kalilou Traore, Mahamane Traore, Mahamadou Samassa (Sigamary Diarra 78), Keita, Diabate.
    Benchi: Mamadou Samassa, N'Diaye, Wague, Maiga, Sissoko, Idrissa Coulibaly, Cheick Diarra, Yatabare, Sow, Samba Diakite, Yirango.
    Kadi ya njano: Tamboura.
    Wafungaji wa mabao: Mahamadou Samassa 21, Keita 48, Sigamary Diarra 90.
    Kikosi cha Ghana: Dauda, Richard Boateng, Vorsah, Boye (Mensah 46), Afful, Wakaso, Awal, Asamoah, Asante, Atsu (Adomah 70), Gyan (Clottey 75).
    Benchi: Agyei, Pantsil, Annan, Agyemang-Badu, Derek Boateng, Rabiu, Akaminko, Boakye, Kwarasey.
    Kadi za njano: Wakaso, Vorsah, Asante.
    Mfungaji wa bao: Asamoah dk82.
    Mahudhurio: 6,000
    Refa: Eric Otogo-Castane (Gabon).
    Mwaka jana, Mali iliifunga Ghana 2-0 katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu. Waliingia kwenye michuano ya mwaka huu wachezaji wakisema wamedhamiria kufanya vizuri ili kuwapa faraja mashabiki wao kwa vurugu za kisiasa zinazoendelea nyumbani kwao. 
    Kipigo cha jana ni pigo lingine kwa Ghana, baada ya kuingia Nusu Fainali kwa mara ya nne mfululizo bila kuingia Fainali. 
    Ghana iliingia kuwania nafasi ya tatu baada ya kutolewa na Burkina Faso kwa mikwaju ya penalti kwenye Nusu Fainali. Black Stars walitwaa taji la mwisho la Mataifa ya Afrika mwaka 1982. 
    Mali ilipania kucheza Fainali kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 30, lakini matumaini yao yalizimwa na kipigo cha 4-1 kutoka kwa Nigeria katika Nusu Fainali.
    Wachezaji wa Mali wanauelekeza ushindi huo kwenye vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini mwao, ambako makundi ya Kifaransa yanapigana na Waislamu. 
    Samassa alifunga kwa kichwa cha mkizi akiwa karibu na eneo la penalty na mchezaji wa zamani wa Barcelona, Keita alifunga bao lake la tatu kwenye mashindano haya akiunganisha krosi kutika wingi ya kulia. 
    Keita alifunga tena dakika ya 72, lakini bao hilo lilikataliwa kwa kuwa tayari kibendera kilikuwa juu, kuashiria alikuwa ameotea. 
    Ghana ilipata bao la kufutia machozi kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa Mali, Soumaila Diakite, ambaye alikuwa shujaa wa timu yake wakiwatoa wenyeji, Afrika Kusini kwa mikwaju ya penakti kwenye Robo Fainali. 
    Cruising: Former Barcelona midfielder Seydou Keita doubled Mali's lead just after half-time
    Kiungo wa zamani wa Barcelona, Seydou Keita akiifungia Mali bao la pili jana
    Again: Mali repeated their 2012 third-place playoff victory over Ghana
    Mali imerudia ubabe wake wa mwaka jana dhidi ya Ghana
    Malian players celebrate
    Joy: Malian fans were also happy with what they saw in Port Elizabeth
    Mali wakishangilia, picha ya juu wachezaji, chini mashabiki

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MALI YAIFUNGA TENA GHANA NA KUTWAA NAFASI YA TATU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top