KIUNGO Jason Puncheon alionyesha ishara ya kutawaza kama mtu aliyemaliza kujisaidia haja kubwa mbele ya mashabiki baada ya kufunga bao la kwanza timu yake Southampton ikiilaza 3-1 Manchester City jana.
Kiungo huyo wa Southampton ni mtu wa mzaha sana na aliwahi kuomba ruhusa ya kutoka uwanjani ili aende chooni mara moja, mechi yao Saints ikirushwa moja kwa moja dhidi ya Everton.
Jason Puncheon akishangilia bao lake dhidi ya Man City
Hivyo, kulikuwa kuna namna moja tu ya Puncheon kushangilia bao lake ufunguzi katika mechi hiyo ya Ligi Kuu.
Puncheon alikimbia upande wa mashabiki wa nyumbani, akainama na kuanza kufanya kama anatawaza.
Puncheon anafunga bao la kwanza