MRENO Cristiano Ronaldo ametoa onyo kali kwa klabu yake ya zamani, Manchester United kwa kufunga mabao matatu peke yake wakati Real Madrid ikipasha misuli kwa ajili ya mechi dhidi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ilipoikung'uta mabao 4-1 Sevilla kwenye Uwanja wa Bernabeu.
Mechi dhidi ya Sevilla have imethibitisha ubora wa Ronaldo na hakuwa na tofauti usiku wa jana akifuatiwa na Karim Benzema, akifunga bao la kwanza dakika ya 18 na mengine dakika za 26, 46 na 59, Madrid wakiibuka washindi.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (katikati) akipongezwa na wenzake Fabio Coentrao na Raul Albiol baada ya kufunga bao dhidi ya Sevilla jana
Ronaldo akifunga bao lake huku amezongwa na beki wa Sevilla, Federico Fazio
Sasa ametimiza Hat-tricks 20 tangu ajiunge na vigogo hao wa Hispania kabla ya kupumzishwa na kocha Jose Mourinho dakika ya 63 kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya United, ambayo itakuwa ya kwanza ya hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Granada, ambayo iliwazima vijana wa Mourinho wiki iliyopita kwa kuwalaza 1-0 kwa bao la Ronaldo kujifunga, imeendeleza ubabe, baada ya kuichapa Deportivo La Coruna mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Riazor.
Bao la kujifunga la Carlos Marchena karibu kabisa na mapumziko liliwatia moto Granada na Ighalo akafunga la pili dakika sita baadaye kipindi cha pili.
Kisha Depor wakapoteza nafasi kadhaa kabla ya kuwapa penalty wapinzani wap- iliyowekwa kimiani na Guilherme Siqueira - dakika ya mwisho huku Manuel Pablo akitolewa nje kwa kadi nyekundu.
"Kwa Madrid kila mechi ni maalum, lakini kwa Jumatano tunapaswa kuwa tayari kukutana na changamoto,"alisema beki wa Madrid, Pepe, aliingia baadaye kucheza mechi yake ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo chake cha mguu wa kulia mapema Januari.
"Cristiano amecheza vizuri. Amepambana sana, tunahitaji aendelee hivyo,".
Ronaldo akikamilisha Hat-trick yake
Ronaldo akishangilia Hat-trick yake ya 20
Ronaldo akifunga kwa mpira wa adhabu