KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameshindwa kumuadhibu mshambuliaji Emmanuel Adebayor licha ya kuchelewa kurudi kwenye timu, baada ya kumaliza majukumu ya kimataifa.
Alimtaka mshambuliaji huyo awasili saa 9:00 Alasiri Ijumaa baada ya Togo kutolewa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na aripoti mazoezini Tottenham.
Togo ilitolewa Jumapili iliyopita, lakini Adebayor alichelewa kujiunga na wenzake mazoezini.
Emmanuel Adebayor hakuwepo mazoezini Tottenham jana, lakini leo kapangwa
Licha ya kuchelewa kuripoti mazoezini, Villas-Boas alimpanga Adebayor katika kikosi cha leo kilichoibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Newcastle katika Ligi Kuu ya England.