• HABARI MPYA

    Monday, February 11, 2013

    MOURINHO: NI MECHI AMBAYO DUNIA INAISUBIRI


    KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba mechi ya wiki hii ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake, Real Madrid na Manchester United 'ni mechi ambayo dunia inaisubuiri'.
    United inakwenda Bernabeu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Jumatano, kabla ya timu hizo kurudiana Old Trafford wiki tatu baadaye, kuamua timu ya kusonga mbele.
    Kikubwa ni kwamba, mwishowe kigogo mmoja ataachia ngazi kwenye masindano katika hatua hii, huku Cristiano Ronaldo akikabiliana na klabu yake ya zamani.
    v
    Cristiano Ronaldo atacheza Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aondoke mwaka 2009

    'Ni mechi ambayo dunia inaisubiri,' Mourinho aliiambia MUTV. 'Watu wanafikiri tupo chini ya shinikizo kwa sababu timu kubwa itatolewa. 'Lakini ni aina ya mechi tunayoitakana watu hawasubiri mechi nyingine yoyote.
    Eager: Mourinho was at Old Trafford to scout Real's opponents
    Mourinho alikuwepo Old Trafford jana kuwasoma wapinzani wake walipocheza na Everton 

    'Natumai tumewapa wanachotaka.'
    Baada ya Ronaldo kufunga Hat-trick nyingine katika ushindi wa Real dhidi ya Seville juzi, Mourinho alisafiri hadi Manchester jana kuitazama United ikiifunga 2-0 Everton Uwanja wa Old Trafford.
    Rivals: But there is a great mutual respect between Ferguson and Mourinho
    Lakini wanaheshimiana sana Ferguson na Mourinho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOURINHO: NI MECHI AMBAYO DUNIA INAISUBIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top