• HABARI MPYA

    Saturday, February 09, 2013

    SIMBA SC NA JKT OLJORO LEO KATIKA PICHA ARUSHA, VILIPIGWA VIATU BALAA

    Eneo la nyavu lililochanwa na shuti la kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha jioni ya leo. Timu hizo zilitoka 1-1.

    Beki wa Oljoro, Salim Mbonde akibutua mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba SC, Mrisho Ngassa katika mchezo huo

    Kiungo wa JKT Oljoro, Kalaghe Gunda akiweka mpira kifuani mbele ya  kiungo wa Simba, Amri Kiemba. Nyuma na beki Nassor Masoud 'Chollo'

    Wachezaji wa Oljoro wakishangilia bao ,ao

    Kipa Said Lubawa wa Oljoro, akiwa amedaka krosi ya Nassor Masoud 'Chollo' (hayupo pichani), huku mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akionekana mwenye kukata tamaa kutokana na ulinzi mkali wa mabeki wa Oljoro

    Beki Salim Mbonde wa Oljoro akiwania mpira, huku akiwa amebanwa na mshambuliaji wa Simba SC, Mrisho Ngassa

    Beki wa Oljoro ameruka juu kuondosha mpira kwenye hatari

    Kocha wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig akikuna pua wakati mchezo ukiendelea

    Wachezaji wa Oljoro wakisali kabla ya mechi

    Amri Kiemba akimtoka beki Saleh Iddi wa Oljoro

    Mwinyi Kazimoto akimtoka beki wa Oljoro, Shaibu Nayopa

    Majaliwa Mbaga wa Oljoro, akiupitia mpira miguu mwa Nassor Masoud 'Chollo'

    Haroun Chanongo akivuta kasi kupiga shuti mbele ya beki wa Oljoro, Majaliwa Mbaga

    Edward Christopher aimtoka beki wa Oljoro 

    Haroun Chanongo akimgeuza beki wa Oljoro, Saleh Iddi

    Rashid Ismail akigombea mpira na beki wa Oljoro, Salim Mbonde mbele ya kipa Said Lubawa

    Amri Kiemba akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Oljoro, Kalaghe Gunda

    Kiungo Jonas Mkude wa Simba kulia akigombea mpira dhidi ya kiungo wa Oljoro

    Mkude amelimwa kwanja hadi chini

    Beki wa Simba, Paul Ngalema akilia kwa uchungu wa maumivu baada ya kutoka nje kufuatia kuumia kwenye mchezo wa leo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC NA JKT OLJORO LEO KATIKA PICHA ARUSHA, VILIPIGWA VIATU BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top