IMEWEKWA MEI 14, 2013 SAA 12:56 ASUBUHI


KIUNGO Mtanzania Adam Nditi jana alirejea uwanjani na kucheza kwa dakika 69 tu wakati timu yake, Chelsea ikifungwa 3-2 na Norwich City katika fainali ya Kombe la FA la Vijana Uwanja wa Stamford Bridge.
Mbaya zaidi Nditi aliwafungia wapinzani moja ya mabao dakika 22, pale alipojifunga katika harakati za kuokoa hivyo kwa pamoja na mabao ya Cameron McGeehan kwa penalti dakika ya 36 na Joshua Murphy dakika ya 75 Norwich iliibuka kidedea.
Nditi alikuwa nje kwa wiki nne kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti na jana ulikuwa mchezo wa kwanza tangu apone na akampisha Wright dakika ya 69.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Jeremie Boga dakika za 15 na 86.
Kikosi cha Chelsea jana kilikuwa: Beeney; Aina/Musonda dk72, Davey, Christiansen, Nditi/Wright dk69; Swift/Colkett dk63, Loftus-Cheek, Baker, Kiwomya, Boga na Feruz.
Norwich: Britt; Norman, McFadden, Toffolo, Wyatt; McGeehan, Randall/Hodd dk90, King/Young dk81, Jacob Murphy, Joshua Murphy na Morris.
Nyota angavu: Cameron McGeehan wa Norwich akishangilia na taji la FA akiwa na wenzake
Nditi akisikitika, huku wachezaji wa Norwich wakishangilia
Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard alishuhudia fainali hiyo
Ashley Cole pia alikuwepo