IMEWEKWA MEI 14,2013 SAA 12:38 ASUBUHI
KLABU ya Manchester City inamuwania winga wa Bayern Munich, Arjen Robben.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 29 anapatikana kwa dau la Pauni Milioni 12, lakini itategemea na City watakavyojidhibiti katika kanuni ya matumizi ya fedha kiungwana.
Anaondoka: Arjen Robben anajiandaa kutemwa na kocha mpya wa Bayern, Pep Guardiola
Robben ana wasiwasi juu ya mustakabali wake kwenye klabu hiyo chini ya kocha mpya Pep Guardiola anayeanza kazi Bayern Munich mwishoni mwa msimu na ameomba kuondoka.
Winga huyo alinunuliwa kwa Pauni Milioni 24 kutoka Chelsea kwenda Real Madrid mwaka 2007, anauzwa katika wakati ambao kocha wa zamani wa Barcelona, Guardiola ameanza mikakati ya kuisuka upya Bayern.
Guardiola hamtaki mchezaji huyo na yupo tayari kusikiliza ofa jambo ambalo litatoa fursa kwa klabu zaidi za Ligi Kuu England kujaribu kumnasa mtaalamu huyo.