IMEWEKWA MEI 15, 2013 SAA 6:30 USIKU


KLABU ya Arsenal imezina furaha ya mabingwa wa Kombe la FA, Wigana mapema zaidi baada ya usiku wa leo kuifungisha virago katika Ligi Kuu ya England kwa kuichapa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Emirates.
Siku tatu tu tangu tu watwae mwali wa FA Jumamosi kwa kuifunga Manchester City katika fainali Uwanja wa Wembley, Wigan leo wamekutana na zahma.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Lukas Podolski dakika ya 11 na 68, Theo Walcott dakika ya 63 na Aaron Ramsey dakika ya 71, wakati la kufutia machozi la Wigan lilifungwa na Maloney dakika ya 45.
Arsenal sasa wanahitaji kuifunga Newcastle Jumapili kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwapiku wapinzani wao, Tottenham, ambao wataangukia nafasi ya tano kwa matokeo yoyote yale katika mchezo wao dhidi ya Sunderland.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta/Vermaelen dk90, Rosicky/Wilshere dk78, Walcott, Cazorla na Podolski/Oxlade-Chamberlain dk78.
Wigan: Robles, Boyce, Scharner, Alcaraz, Espinoza, McManaman/Di Santo dk57, Maloney/Henriquez dk85, McCarthy, McArthur, Kone na Gomez/Watson dk64.
wakati wa kuiaga Ligi Kuu: Wigan watacheza Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship msimu ujao
Mtunguo: Lukas Podolski akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Wigan
Theo Walcott akishangilia kuifungia The Gunners