IMEWEKWA MEI 15, 2013 SAA 7: 54 USIKU
SIKU moja baada ya Roberto Mancini kutupiwa virago Manchester City, timu hiyo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini Uwanja wa Madejski dhidi ya wenyeji Reading, klabu ambayo amewahi kuchezea kipa Mtanzania, Mwameja Mohamed ikiwa Daraja la Tatu.
Ikiwa chini ya aliyekuwa msaidizi wa Mancini, Brian Kidd, Man City leo ilipata mabao yake kupitia kwa Aguero dakika ya 40 na Dzeko dakika ya 88.
Kikosi cha City, leo kilikuwa; Hart, Richards, Toure/Maicon dk15, Lescott, Clichy, Toure, Barry/Garcia dk58, Milner, Silva, Tevez na Aguero/Dzeko dk62.
Reading: McCarthy, Gunter, Morrison, Mariappa, Kelly, Karacan, Guthrie, McCleary, McAnuff/Blackman dk69, Robson-Kanu, Pogrebnyak/Le Fondre dk62.
Mwanzo mzuri: Brian Kidd ameiongoza City kushinda mechi ya kwanza chini yake kama kocha wa muda
Aguero aliifungia bao la kwanza City.