• HABARI MPYA

    Monday, May 13, 2013

    BALOTELLI ASABABISHA MECHI YA AC MILAN KUSIMAMA ITALIA...CHUPUCHUPU IVUNJIKE MOJA KWA MOJA, AMPONZA MUNTARI KULIMWA KADI NYEKUNDU


    IMEWEKWA MEI 13, 2013 SAA 12:15 ASUBUHI
    MECHI ya AC Milan ya Serie A usikuwa jana ilisimama kwa muda kwa sababu kejeli za kibaguzi ambazo zilielekezwa kwa Mario Balotelli na wachezaji wengine weusi kutoka kwa mashabiki wa Roma. 
    Refa Gianluca Rocchi alisimamisha mechi na mtangazaji wa uwanjani akawaambia mashabiki wa Roma waache kuwafanyia ishara za nyani wachezaji weusi wa Milan, vinginevyo mechi itaahirishwa.
    Mapema Sulley Muntari alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati anakwenda kumsihi refa huyo aliyeonekana aataka kumpa kadi ya pili ya njano Balotelli.
    Disgrace: Roma fans aimed racist abuse at Mario Balotelli
    Dharau: Mashabiki wa Roma walimkejeli Mario Balotelli kwa rangi yake
    Halted: Balotelli and Kevin Prince-Boateng stand together during the stadium announcement
    Inauma: Balotelli na Kevin Prince-Boateng wakiwa wamesimama pamoja wakati wa tangazo linatolewa uwanjani
    Players wait for the game to be resumed
    Nahodha wa Roma, Francesco Totti na wachezaji wa Milan

    Massimo Ambrosini alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kulalamika kwa refa Rocchi kabla ya mechi kusimamishwa.
    Totti baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu beki wa Milan, Phillipe Mexes na mechi hiyo ikaisha kwa sare ya bila kufungana.
    Mchezo wa kirafiki Januari baina ya Milan na Pro Patria ulisimamishwa pia kwa sababu kejeli za kibaguzi alizofanyiwa Kevin-Prince Boateng.
    Shirikisho la soka Italia limeweka sheria mpya kuwasaidia marefa kudhibiti ubaguzi baada ya kiungo wa Milan, Kevin-Prince Boateng kuamua kuondoka uwanjani January katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria baada ya kukutana na dhalili hiyo.
    Dismissed: Sulley Muntari was sent off for restraining the referee
    Anatolewa nje: Sulley Muntari alitolewa nje kwa kumsihi refa

    Marefa sasa wana uwezo wa kuvunja mechi yakitokea mambo ya kibaguzo uwanjani kwa kutoa tangazo kabla ya kuchukua hatua hiyo.
    You're off: Totti was dismissed for a vicious elbow on Phillipe Mexes
    Unakwenda nje: Totti alitolewa na refa kwa kumchezea rafu  Phillipe Mexes
    Hold up: The game was nearly postponed because of the abuse
    Mechi imesimama: mchezo ulisimama kwa muda sababu ya ubaguzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BALOTELLI ASABABISHA MECHI YA AC MILAN KUSIMAMA ITALIA...CHUPUCHUPU IVUNJIKE MOJA KWA MOJA, AMPONZA MUNTARI KULIMWA KADI NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top