• HABARI MPYA

    Monday, May 13, 2013

    MECHI 25 ZA KASEJA DHIDI YA WATANI WA JADI, JUMAMOSI NI YEYE TENA TAIFA NA YANGA?


    NA MAHMOUD ZUBEIRY, IMEWEKWA MEI 13, 2013 SAA 12:25 ASUBUHI
    NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zinatarajiwa kuwaka moto Jumamosi wiki hii (Mei 18, 2013) kwa mpambano wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga. Huo utakuwa mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wakiwa tayari wamewavua ubingwa wapinzani wao wa jadi, Simba SC. Kuanzia leo, BIN ZUBEIRY itakuwa ikikuletea mfululizo wa makala za kuelekea pambano hilo linalobeba picha halisi ya soka ya Tanzania. Kwa leo, tunaanza na kipa gwiji, Juma Kaseja Juma juu ya mapambano ya watani. Endelea.
    Kocha Mfaransa, Patrick Liewig ametokea pia kumuanini zaidi Kaseja mbele ya Dhaira

    KAMA Jumamosi atasimama kwenye milingoti mitatu, Juma Kaseja atatimiza mechi 26 za wapinzani wa jadi katika soka ya Tanzania kucheza, tangu ajiunge na Simba mwaka 2003, kati ya hizo moja tu, akiidakia Yanga mwaka 2009.
    Kama itakumbukwa Kaseja, alisajiliwa Simba mwishoni mwa mwaka 2002, akitokea Moro United na moja kwa moja akaachiwa mikoba na aliyekuwa Simba One, Mwameja Mohamed. 
    Kwa kuwa Mwameja alikuwa Tanzania One pia, haikuchukua muda, Kaseja naye akawa Tanzania One, akirithi mikoba ya Manyika Peter, aliyekuwa kipa wa Yanga. Makipa wote hawa watatu, Mwameja, Manyika na Kaseja walikuwa mahiri wa kuokoa mikwaju ya penalti. 
    Mechi ya kwanza ya watani Kaseja kucheza ilikuwa Aprili 20, mwaka 2003 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ambayo Yanga ilishinda 3-0, mabao yake yakifungwa na Kudra Omary dakika ya 30, Heri Morris dakika ya 32 na Salum Athumani dakika ya 47.
    Hii ilikuwa mechi maalum ya kirafiki, iliyoandaliwa na promota Dika Sharp kwa kushirikiana na Prime Time Promotions, ambayo ilipewa jina ‘Big Match’
    Mechi ya pili ikafuatia Septemba 28, mwaka 2003, katika Ligi Kuu ambayo iliisha kwa sare ya 2-2, mabao ya Simba yakifungwa na Emmanuel Gabriel dakika ya 27 na 36, wakati ya Yanga yalifungwa na Kudra Omary dakika ya 42 na Heri Morris dakika ya 55.
    Mechi ya tatu ilikuja Novemba 2, mwaka 2003 ya Ligi Kuu, marudiano ambayo iliisha kwa sare ya bila kufungana. 
    Mechi ya nne iliikuja Agosti 7, mwaka 2004, ilikuwa ya Ligi Kuu pia, Simba ikashinda 2-1, mabao ya Shaaban Kisiga ‘Malone’ dakika ya 64 na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 76, wakati la Yanga lilifungwa na Pitchou Kongo dakika ya 48.
    Mechi ya tano ilikuja Septemba 18, mwaka 2004 ya Ligi Kuu pia, bao pekee la Athumani Machuppa dakika ya 82, likiipa ushindi Simba.
    Mechi ya sita ilikuja Aprili 17, 2005 na Simba ikashinda tena 2-1, Ligi Kuu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, mabao yake yakifungwa na Nurdin Msiga dakika ya 44 na Athumani Machupa dakika ya 64, baada ya Aaron Nyanda kutangulia kuifungia Yanga dakika ya 39.
    Mechi ya saba, ilikuja Julai 2, mwaka 2005 ya fainali ya Kombe la Tusker, ilichezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Yanga ikalala 2-0, mabao ya Emmanuel Gabriel dakika ya 60 na Mussa Hassan Mgosi dakika ya 72.
    Mechi ya nane ilikuja Agosti 21, mwaka 2005 ya Ligi Kuu, ambayo Simba ilishinda 2-0, mabao yote yakitiwa kimiani na Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nico Nyagawa katika dakika za 22 na 56 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
    Mechi ya tisa ilikuja Machi 26, mwaka 2006 ya Ligi Kuu, lakini hiyo iliisha kwa sare ya bila kufungana na mechi ya 10, ilikuja Agosti 15, mwaka 2006, Nusu Fainali ya Kombe la Tusker, ambayo iliisha kwa sare ya 1-1, Emanuel Gabriel akitangulia kuifungia Simba dakika ya 69 na Credo Mwaipopo akaisawazishia Yanga dakika ya 90. Simba ikashinda kwa penalti 7-6.
    Mechi ya 11 ilikuja Oktoba 29, mwaka 2006, Ligi Kuu ambayo iliisha kwa sare tasa, yaani 0-0 na mechi ya 12 ilikuja Julai 8, mwaka 2007, Fainali ya Ligi Ndogo, ambayo matokeo yalikuwa 1-1 ndani ya dakika 120, Moses Odhiambo akitangulia kuifungia Simba penalti dakika ya pili, kabla ya Said Maulid ‘SMG’ kusawazisha dakika ya 55 na Simba ikashinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Mechi ya 13, ilikuja Oktoba 24, mwaka 2007, Ligi Kuu na ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na bao pekee la Ulimboka Mwakingwe, dakika ya 14, lilipa Simba ushindi. Mechi ya 14 ilikuja Aprili 27, ya Ligi Kuu pia, mwaka 2008, ambayo iliisha kwa sare ya bila kufungana, wakati mechi ya 15, ilikuja Aprili 19, mwaka 2009, Juma Kaseja akiwa katika mkataba wa mwaka na Yanga. 
    Aliidakia Yanga siku hiyo na mechi hiyo ya Ligi Kuu ikaisha kwa sare ya 2-2, mabao ya Simba yakifungwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dakika ya 23 na Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 62, wakati ya Yanga yalifungwa na Ben Mwalala dakika ya 48 na Jerry Tegete dakika ya 90.
    Mechi ya 16 ilikuja Oktoba 31, mwaka 2009, Kaseja akiwa tayari amerejea Simba SC na akaiongoza timu yake kipenzi kuilaza Yanga 1-0, bao pekee la Mussa Hassan Mgosi dakika ya 26 katika Ligi Kuu.
    Mechi ya 17, ilikuja Desemba 25, mwaka 2009, Nusu Fainali ya Kombe la Tusker na Yanga ilishinda 2-1, mabao ya Jerry Tegete dakika ya 67 na Shamte Ally dakika ya 120, wakati la Simba lilifungwa na Hillary ‘Ford’ Echesa dakika ya 78 kwa penalti.
    Mechi ya 18, ilikuja Aprili 18, mwaka 2010 na Yanga ilichapwa mabao 4-3, Ligi Kuu pia, mabao ya Simba yakifungwa na Uhuru Suleiman dakika ya tatu, Mussa Mgosi dakika ya 53 na 74 na Hillary Echesa dakika ya 90 na ushei, wakati ya wana Jangwani, yalifungwa na Athumani Iddi ‘Chuji’ dakika ya 30, Jerry Tegete dakika ya 69 na 89.
    Mechi ya 19 ilikuja Oktoba 16, mwaka 2010, Ligi Kuu pia, Yanga ikishinda 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, bao pekee la Jerry Tegete dakika ya 70, wakati ya mechi ya 20 iliyokuja Machi 5, mwaka 2011, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Stefano Mwasyika akitangulia kuifungia Yanga kwa penalti dakika ya 59, kabla ya Mussa Mgosi kuisawazishia Simba dakika ya 73, ilikuwa ya Ligi Kuu pia.

    Mechi ya 21 ilikuja Julai 10, mwaka 2011, Yanga ilishinda 1-0, Fainali Kombe la Kagame, mfungaji Mghana Kenneth Asamoah dakika ya 108, wakati mechi ya 22 ilikuja Agosti 17, mwaka 2011, Simba ikishinda 2-0, mabao ya Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 15 na Felix Sunzu dakika ya 38 kwa penalti, kuwania Ngao Jamii.
    Mechi ya 23 ilikuja Oktoba 29, mwaka 2011 na Yanga ikashinda 1-0, bao pekee la Davies Mwape dakika ya 75, Ligi Kuu pia, wakati mechi ya 24 ni ile ya 5-0, Mei 6, mwaka 2012, Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Emmanuel Okwi dakika ya pili na 62, Felix Sunzu kwa penalti dakika ya 56, Juma Kaseja kwa penalti dakika ya 67 na Patrick Mafisango (marehemu) kwa penalti pia dakika ya 72. 
    Mechi ya 25 na ya mwisho Kaseja kudaka ilikuwa ya Oktoba 3, mwaka jana timu hizo zikitoka sare ya 1-1 katika Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, tena Yanga wakikomboa bao kwa penalti kupitia kwa Said Rashid Bahanuzi dakika ya 65, baada ya Amri Kiemba kutangulia kufunga dakika ya tatu.   
    Ingawa kwa sasa Simba SC inaye kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira lakini unapozungumzia mapambano ya watani, bado rekodi inambeba Kaseja kusimama kwenye milingoti mitatu Jumamosi na akidaka siku hiyo, itakuwa mechi ya 26, nani kama Kaseja?
    Kaseja atadaka mechi ya 26 ya watani Jumamosi?


    MECHI ZA WATANI ALIZOCHEZA KASEJA:
    APRILI 20, 2003,
    CCM Kirumba, Mwanza
    Yanga Vs Simba 3-0
    WAFUNGAJI:
    Kudra Omary dk. 30, Heri Morris dk 32 na Salum Athumani dk. 47
    (Mechi ya kirafiki iliandaliwa Dika Sharp, CCM Kirumba Mwanza)
    SEPTEMBA 28, 2003
    Simba v Yanga
    2-2
    WAFUNGAJI:
    Simba: Emmanuel Gabriel dk. 27 na 36
    Yanga: Kudra Omary dk. 42, Heri Morris dk. 55
    (Ligi Kuu)
    NOVEMBA 2, 2003
    Simba v Yanga
    0-0
    (Ligi Kuu)
    AGOSTI 7, 2004
    Simba v Yanga
    2-1
    WAFUNGAJI:
    Simba: Shaaban Kisiga dk. 64, Ulimboka Mwakingwe dk. 76
    Yanga: Pitchou Kongo dk. 48
    (Ligi Kuu)
    SEPTEMBA 18, 2004
    Simba v Yanga
    1-0
    MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk. 82
    (Ligi Kuu)
    APRILI 17, 2005
    Simba v Yanga
    2-1
    WAFUNGAJI:
    Simba: Nurdin Msiga dk. 44, Athumani Machupa dk. 64,
    Yanga: Aaron Nyanda dk. 39
    (Ligi Kuu, ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)
    JULAI 2, 2005
    CCM Kirumba, Mwanza. Fainali
    Simba Vs Yanga, 2-0
    WAFUNGAJI: Emmanuel Gabriel dk. 60, Mussa Hassan Mgosi dk. 72
    (Ligi Kuu)
    AGOSTI 21, 2005
    Simba v Yanga
    2-0
    MFUNGAJI: Nico Nyagawa dk. 22 na 56
    (Ligi Kuu, ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)
    MACHI 26, 2006
    Simba v Yanga.
    0-0
    (Ligi Kuu)
    AGOSTI 15, 2006
    Simba Vs Yanga; Nusu Fainali, 1-1
    WAFUNGAJI:
    SIMBA: Emanuel Gabriel dk. 69
    YANGA: Credo Mwaipopo 90
    (Kombe la Tusker, Simba ilishinda kwa penalti 7-6)
    OKTOBA 29, 2006
    Simba v Yanga
    0-0
    (Ligi Kuu)
    JULAI 8, 2007
    Simba v Yanga
    1-1 (dakika 120)
    WAFUNGAJI:
    Simba: Moses Odhiambo (penalti dk. 2)
    Yanga: Said Maulid (dk. 55).
    (Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo).
    (Fainali, Ligi Ndogo, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)
    OKTOBA 24, 2007:
    Simba Vs Yanga
    1-0
    Mfungaji: Ulimboka Mwakingwe
    (Ligi Kuu, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)
    APRILI 27, 2008:
    Simba Vs Yanga
    0-0
    (Ligi Kuu)
    APRILI 19, 2009
    Simba Vs Yanga
    2-2
    WAFUNGAJI:
    SIMBA: Ramadhan Chombo dk 23, Haruna Moshi dk 62
    YANGA: Ben Mwalala dk48, Jerry Tegete dk90
    (Ligi Kuu, Kaseja alidakia Yanga)
    OKTOBA 31, 2009
    Simba Vs Yanga
    1-0
    MFUNGAJI: Mussa Hassan Mgosi dk 26
    (Ligi Kuu)
    DESEMBA 25, 2009
    Yanga Vs Simba; Nusu Fainali, 2-1
    WAFUNGAJI:
    YANGA: Jerry Tegete dk 67, Shamte Ally dk 120
    SIMBA: Hillary Echesa dk 78 (penalti)
    (Kombe la Tusker)
    APRILI 18, 2010
    Simba Vs Yanga
    4-3
    WAFUNGAJI:
    SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+ 
    YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89
    (Ligi Kuu)
    OKTOBA 16, 2010:
    Yanga Vs Simba
    1-0
    MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70
    (Ligi Kuu)
    MACHI 5, 2011
    Simba Vs Yanga
    1-1
    WAFUNGAJI:
    YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.
    SIMBA:  Mussa Mgosi dk 73.
    (Ligi Kuu).
    JULAI 10, 2011
    Yanga 1-0 Simbam, Fainali
    MFUNGAJI : Kenneth Asamoah dk 108
    (Kombe la Kagame)
    AGOSTI 17, 2011
    Simba vs Yanga 2-0, Dar
    WAFUNGAJI:
    Haruna Moshi ‘Boban’ dk 15 na Felix Sunzu dk 38.
    (Ngao ya Jamii)
    OKTOBA 29, 2011
    Yanga 1-0 Simba
    MFUNGAJI: Davies Mwape dakika ya 75
    (Ligi Kuu)
    MEI 6, 2012
    Simba 5-0 Yanga SC
    WAFUNGAJI: 
    Emmanuel Okwi (dk 2 na 62), Felix Sunzu (penalti 56), Juma Kaseja (penalti dk 67) na Patrick Mafisango (penalti dk 72)
    (Ligi Kuu)
    OKTOBA 3, 2013
    Simba 1-1 Yanga SC
    WAFUNGAJI:
    Simba SC: Amri Kiemba dk3
    Yanga SC: Said Bahanuzi dk65
    (Ligi Kuu)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MECHI 25 ZA KASEJA DHIDI YA WATANI WA JADI, JUMAMOSI NI YEYE TENA TAIFA NA YANGA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top