• HABARI MPYA

    Monday, May 13, 2013

    COCA COLA YAGAWA VIFAA KWA AJILI YA COPA COCA COLA 2013

    Kulia ni Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka akimkabidhi Ofisa Maendeleo ya soka wa TFF, Salum Madadi vifaa vya michezo kwa ajili ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki


    Na Prince Akbar, IMEWEKWA MEI 13, 2013 SAA 5:50 ASUBUHI
    KAMPUNI ya Coca-Cola imelikabidhi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mipira na bips kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu yatakuwa ya umri chini ya miaka 15 badala ya chini ya miaka 17 kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
    Lengo la kubadili umri kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ni kuweza kuwafikia vijana wadogo zaidi na hivyo kuwa na wigo mpana wa kukuza vipaji vyao kwa muda mrefu zaidi kabla hawajachukuliwa na vilabu vikubwa.
    Vifaa vilivyotolewa na Coca-Cola na kupokelewa na Ofisa Maendeleo ya soka wa TFF, Salum Madadi vitatumika ngazi ya wilaya. Akipokea vifaa hivyo, kocha huyo wa zamani wa Simba SC na Taifa Stars, amewataka viongozi wa soka ngazi ya wilaya na mikoa kuzingatia kanuni na taratibu za Copa Coca-Cola. Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika ofisi za Coca-Cola Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
    Alisema kuwa baadhi ya wilaya tayari zimeshaanza mechi za michuano hiyo ya vijana na kuzitaka wilaya ambazo zilikuwa zinasubiri vifaa ili kuanza kucheza kufanya hivyo mara moja kwa kuwa sasa vifaa viko tayari. 
    Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania  Maurice Njowoka alisistiza msimamo thabithi wa Coca-Cola wa kuendelea kudhamini mashindano ya Copa Coca-Cola ambayo yamekuwa chimbuko la wanasoka chipukizi nchini Tanzania.
    “Tumeamua kubadili mashindano ya Copa Coca-Cola kuwa ya umri chini ya miaka 15 badala ya chini ya umiri wa miaka 17 kama ilivyokuwa miaka iliyopita ili kutoa fursa kwa vijana wadogo zaidi kufundishwa na kuendeleza vipaji vyao na kupata uzoefu mapema zaidi,” alisema Njowoka.
    Barani Afrika, mashindano ya soka ya vijana ya Copa Coca-Cola hufanyika katika nchi zaidi ya 20 na kushirikisha zaidi ya wachezaji chipukizi zaidi ya 50,000. Miaka iliyopita Copa Coca-cola imeweza kuibua vipaji vya wachezaji nyota ikiwa ni pamoja na mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Zambia Kennedy Mweene na wachezaji wenginie Nathan Sinkala na tophila Sunzu; Uganda ni pamoja na mlinzi wa kimataifa Timothy Batabaire; Nigeria ni kiungo wa FC Porto Mikel Agu; Kenya ni kiungo mahili Donald Mariga; Tanzania ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu; na Afrika Kusini Mandla Masango na Happy Jele. Hawa ni kwa uchache tu.
    “Tuna nyota wengi wanaoibuka kutokana na mashindano ya Copa Coca-Cola kila mwaka,” anasema Njowoka. “Wachezaji waliofanikiwa wamekuwa ni chachu ya sisi kujisikia fahari na kuendelea kudhamini mashindano hayo. Wachezaji wanaojituma na kufanikiwa ni mashujaa. Wazazi wanaowapa moyo vijana wao na kuwaongoza ni mashujaa. Makocha wanaojitoa kwa moyo mmoja kufundisha vijana ni mashujaa. Hata washabiki wanaojitokeza kuwatia moyo wachezaji pia ni mashujaa. Hii inakuwenda sanjali na kauli mbiu yetu kwamba Copa Coca-cola ni mashindano yanazaa mashujaa,” alisema.
    Mashindano ya mwaka huu yanafuatia ya mwaka jana yaliyofana katika nchi zaidi ya 20 barani Afrika ambapo vijana 134 walipata fursa ya kwenda Afrika Kusini kushiriki kambi ya mafunzo ya soka kwa wiki mbili 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: COCA COLA YAGAWA VIFAA KWA AJILI YA COPA COCA COLA 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top