MEI 8, 2013
KLABU ya Atletico Madrid inaendelea kufuatilia nafasi ya Luis Suarez katika klabu ya Liverpool wakimfikiria akazibe pengo la Radamel Falcao.
Klabu hiyo ya Hispania ni moja kati ya klabu kubwa Ulaya zinamzotaka yota huyo wa Uruguay, ambaye bado hajatoa msimamo wake kama atabaki au ataondoka Liverpool msimu ujao.
Suarez atakosa mechi sita za mwanzoni msimu ujao na Liverpool ina wasiwasi baada ya adhabu yake ya kumng'ata Branislav Ivanovic atataka kuondoka England mwishoni mwa msimu.
Yuko njiani? Luis Suarez anatumikia adhabu ya kusimamishwa kwa mechi 10 baada ya kumng'ata Branislav Ivanovic
Suarez (kulia) anaweza kurithi mikoba ya Mcolombia Radamel Falcao (kushoto) akiondoka
Bayern Munich na Juventus zinaandaa ofa, lakini Atletico imekuwa ikijiandaa kwa mwaka wote huu kuishi bila nyota huyo, Falcao anayetakiwa na Chelsea pia.
Atletico inao wachezaji wengine wawili wa Uruguay, Diego Godin na Cristian Rodriguez wote rafiki wa Suarez.