IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
KLABU ya Arsenal imehamishia ndoana zake kwa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez.
Kocha Arsene Wenger amefanya hivyo akiwa tayari ana mpango wa kuwasajili washambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney na wa Real Madrid, Gonzalo Higuain.
Harakati za kumnasa Suarez ahamishie makali yake Arsenal zilianza wiki iliyopita.
Anatakiwa: Arsenal imeomba kumsajili nyota wa Liverpool, Suarez, raia wa Uruguay ambaye anataka kuondoka Anfield
Wanatakiwa pia: Tayari kuna mezani kwa ajili ya Higuain (kushoto), wakati uhamisho wa Rooney (kulia) unaonekana kuwa mgumu
Pamoja na hayo, Liverpool haijapokea ombi lolote rasmi na inabaki na msimmo wake kwamba Suarez anatakiwa kuwasilisha maombi ya kuondoka kama anataka kuhama.
Wanatarajia kuzungumza zaidi na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wiki hii. Amekakaririwa mara kadhaa na vyombo vya Habari vya Uruguay na Hispania juu ya ya nia yake ya kuondoka England na Real Madrid inabakia kuwa klabu inayopewa nafasi zaidi ya kumnasa.
Chelsea ilihusishwa na mpango wa kumchukua mchezaji huyo wiki iliyopita na vyombo vya Habari vya Hispania, lakini wenyewe wanahangaikia saini za wachezaji wengine.
Anapagawisha: Suarez alihusishwa na kuhamia Chelsea wiki iliyopita na vyombo vya Habari vya Hispania
Kuhamia klabu nyingine England linachukuliwa kama jambo ambalo Suarez hapendi, kutokana na ukweli kwamba anaamini hapendwi England na ndiyo maana akafungiwa mechi 10 kwa kumng'ata Branislav Ivanovic, na Arsenal kumfuata Gonzalo Higuain wanaamini mchezaji huyo atahamia Hispania.
Higuain ameanza mazeozi ya kujiandaa na msimu mpya na Madrid na klabu yake inataka Pauni Milioni 27 ili kumuuza Muargentina huyo Arsenal ili apate fedha za kuipa Real Sociedad kwa ajili ya Asier Illaremendi.
Wakati huo huo, Liverpool inamtaka kiungo wa Verona, Mbrazil, Jorginho, mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia anatakiwa na AC Milan.
Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili beki anayetakiwa na Liverpool, Tiago Ilori kutoka Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 20.
Anatakiwa: Liverpool inasotea saini ya Llori (kushoto), na Chelsea nayo sasa inamuwania
Mmoja chini: Moyes anaweza kuwa amekwishashinda vita ya kumbakiza Wayne Rooney Old Trafford