IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 11:28 ALFAJIRI
WAKATI anafungua Mkutano Mkuu maalum wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana kwenye ukumbi wa Water Front, Dar es Salaam, Mkuu Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema Tanzania inatembea na falsafa ya matokeo makubwa sasa kuelekea kujikuza kiuchumi hadi kiwango cha kati.
Bendera, ambaye pia ni kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alisema nchi ipo katika kipindi cha marekebisho ili iwe na uchumi wa kati na ndiyo maana Watanzania wote hivi sasa wanatakiwa wawe na fikra za kukimbia badala ya kutembea.
“Nchi yetu ina falsafa ya big results now (matokeo makubwa sasa). Nchi yetu inaweka vipaumbele sita, ambavyo ni umeme, Reli na barabara, Kilimo, Elimu, Maji na Fedha.
“Fedha inayohitajika ni shilingi Trilioni 3.9 kwa kipindi cha miaka mitatu tu, sasa kwa kuzingatia hilo, nasi katika soka lazima tuwe na big results now. Ni wakati sasa wa kuinua kiwango chetu cha soka nchini kote. Hatutapiga hatua kama tutaendeleza maadui hawa watatu. Fitina, Majungu na Umbeya,”alisema.
Baadaye jioni akaibuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baada ya dakika 90 akaondoka kinyoge kutokana na Taifa Stars kufungwa 1-0 na Uganda, The Cranes, bao pekee la Dennis Iguma dakika ya 46 katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Iguma aliifungia The Cranes bao hilo, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Stars kufuatia krosi maridadi ya Brian Majwega, ambaye jana alikuwa mwiba mkali kwa Taifa Stars.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na kwa ujumla katika dakika zote hizo 45 hakukuwa na shambulizi la kutisha kwa pande zote.
Brian Majwega alifanikiwa kumgeuza uchochoro Erasto Nyoni na kuingia ndani mara kadhaa, lakini pasi na krosi zake ziliokolewa na mabeki wa Stars inayofundishwa na Mdenmark, Kim Poulsen.
Mrisho Ngassa alipewa mipira mirefu kadhaa, lakini mabeki wa Uganda wakiongozwa na mkongwe, Nahodha wao, Hassan Wasswa walisimama imara kumdhibiti.
Mashambulizi mengine ya Stars yalipitia kwa John Bocco ‘Adebayor’, ambaye alikuwa anapigiwa mipira mirefu, lakini alidhibitiwa pia. Timu zote zilicheza sawa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko, Stars ikiwapumzisha beki Erasto Nyoni na kiungo Mwinyi Kazimoto na kuwaingiza David Luhende na Haroun Chanongo, lakini walikuwa ni Uganda wanaofundishwa na makocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ anayesaidiwa na Sam Timbe waliobuka vinara.
Lakini baada ya kufungwa Stars, waliongeza kasi na nguvu ya uchezaji na kufanikiwa tu kulitia misukosuko lango la Uganda na si kupata bao japo la kusawazisha.
Matokeo hayo yanamaanisha Stars itahitaji kushinda ugenini kuanzia mabao 2-0 wiki mbili zijazo ili isonge mbele, vinginevyo itakuwa imetupwa nje ya mashindano hayo.
Kwa kweli matokeo ya jana yameumiza na kikubwa ni kufungwa nyumbani, tena na timu ambayo si ya kutisha, Uganda iliyoshuka jana Uwanja wa Taifa, haikuwa ya kutufunga na pamoja na ukweli kwamba soka ni mchezo wa bahati wakati mwingine, lakini kuna makosa yalifanyika na kubwa ni kujiamini kupita kiasi.
Wachezaji wetu na benchi lao la Ufundi, baada ya kuonyesha soka nzuri katika mechi kadhaa zilizopita za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia, japokuwa hawakupata matokeo mazuri sana, wakaona sasa tayari wao ni wa kiwango kingine.
Kocha wa Uganda, Milutin Sredojevich ‘Micho’ naye akawavimbisha vichwa aliposema kikosi cha Stars ni kile kile kilichocheza na Ivory Coast, kasoro wachezaji wawili tu, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, hivyo anawapa nafasi kubwa ya kushinda.
Stars iliwadharau Uganda- na hata mashabiki wengi wao walikwenda uwanjani kwa mtazamo wa kushangilia mabao. Walikuwa wamekwishabeba taswira za Mrisho Ngassa na Amri Kiemba wakishangilia mabao.
Rejea zile dakika takriban 30 za mwisho, Stars ikiwa imekwishalala 1-0 namna timu ilivyobadilika na kucheza kwa juhudi kusaka bao la kusawazisha na pale ilikosekana bahati tu, lakini wangeweza kupata japo bao moja.
Uganda walijua, Tanzania wataamka na kusaka mabao- wakawa makini mno. Kocha anajua makosa yake yaliyochangia matokeo mabaya jana, kuanzia katika kuiandaa timu, kuipanga, mfumo wa uchezaji na hata kuiongoza katika mchezo wa jana. Kadhalika na wachezaji. Marefa hawakuwa wabaya upande wetu, zaidi walitufanyia uungwana na kulea rafu za kipumbavu zilizochezwa na wachezaji wetu.
Lakini bado Stars inatia matumaini, ndani ya wachezaji wote alionao kambini sasa, kama Kim Poulsen atafanyia kazi makosa yote, kuanzia upangaji wa timu, mfumo wa uchezaji na namna ya kuiongoza timu, kuhakikisha anakuwa na mbinu za ziada za mchezo na si kutegemea ile ile aliyoingia nayo hata kama imefeli, basi uwezekano wa kwenda Afrika Kusini upo.
Uwanja wa Namboole ni kama wa Taifa tu. Na Stars imekwishacheza hapo mara kadhaa hapatawasumbua. Kim na vijana wake hawahitaji kukata tamaa. wanatakiwa kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano, ambao lazima washinde ugenini ili kukata tiketi ya CHAN. Na inawezekana.
Ila kwa jana, kujiamini kupiota kiasi kuliiponza Stars ikafungwa na Uganda nyumbani.